Kwa kweli maisha ya Mtume Muhammad s.a.w. yameandikwa kwa mashairi ya Kiswahili na watu kadhaa wa kadhaa, miongoni mwao ni Sayyid Abu Bakar bin Abdulrahman (Mwenye Mansabu) aliye kuwa mwanazuoni mkubwa, Kadhi na mshairi mkubwa wa Lamu, Sheikh Mzee bin Ali Comorian wa Dar es Salaam na Shekh Saidi Musa wa Dar es Salaam. Lakini hao wote wameifasiri ile ile Maulidi ya Barzanji. Zipo na tenzi nyengine ambazo hazikutegemezwa juu ya Maulidi ya Barzanji lakini nazo ni fupi kabisa.
Utenzi huu wa Ruwaza Njema
(Uswatun Hasana) ni wa kwanza katika tenzi juu ya maisha ya Mtume s.a.w.
ulioandikwa kwa urefu na ukamilifu
Sifa kuu ya utenzi huu ni jitihada ya mtungaji kuandika ambalo
ameyakinika nalo kuwa ni sahihi, la kweli tu, na halina
khtilafu. Hilo si jambo jepesi kwa watungaji tenzi,
kwani wao mara nyingi huvutika kwa utamu wa ushairi wakapita mpaka katika
kusifu au kushutumu. Mwenye kusoma utenzi huu, kama
mwenye kusoma kitabu changu Maisha ya Nabii Muhammad naayakinike kuwa
anasoma mambo yaliyothibiti katka taarikh (historia), wala hapana uzushi.
Kitabu changu kimepigwa chapa mara nyingi, na kila mara nakla zote
zilimalizika. Nina tamaa kubwa kuwa utenzi huu utapendwa
kama kilivyopendwa kitabu changu, au pengine na kuzidi, kwani nudhumu ya
mashairi huvutia zaidi kuliko maandishi ya sesa (ya "nathari").
Katika sifa za utenzi huu ni kuwa umezidi kuweka wazi na kutiltia
mkazo yale mambo katika maisha ya Mtume s.a.w. ambayo ni muhimu sana katika
kutuongoza sawa sisi Waislamu katika maisha yetu ya Afrika
Mashariki. Ustahamilvu, kusubiri kwa misiba, ushujaa kwa
kupigania haki, uadilifu katika kutawala na kuhukumu, kuondoa ubaguzi wa rangi
na kabila, kujenga umoja, ukarimu na kuwania kheri ya wenzako kuliko kuwania
maslaha ya binafsi - yote haya, na kama haya, yafaa sana sisi tujifunze katika
maisha ya mtu huyu wa ajabu, Nabii Muhammad s.a.w.
Katika kitabu hichi tuna bahati nzuri kuwa mwenyewe mtungaji
ametuwekea maelezo yake, kwa hivyo tunaweza kuyaelewa makusudio yake bila ya
taabu. Katika hayo maelezo pia ametia ushahidi na uthibitisho kwa lolote katika
fikra zake ambazo huenda zikaleta makindano yoyote. Kwa fikra zake ambazo
huenda zikakhitalifiana na maoni yangu pia namhishimu, kwa sababu amezitolea
hoja kwa kadri ya uwezo wake. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kabisa.
Aghlabu ya Waafrika ni wafuasi wa Mtume Muhammad s.a.w. Uislamu umeliathiri Bara hili kuliko mabara yote. Na haya si ajabu, kwani Uislamu ulifika Afrika Mashariki kabla ya kuenda Arabuni kote, bali hata kabla ya kufika Madina. Kwani walipokuwa wanateswa sana Waislamu, Mtume s.a.w. aliwaamuru baadhi ya wafuasi wanyonge wakimbilie Uhabeshi. Hapo ilikuwa ni miaka minane kabla ya Madina kusilimu. Pia miongoni mwa Waislamu wa mwanzo ni Waafrika Mashariki, kama Bwana Bilal r.a. na Mama Baraka r.a. mlezi wake Mtume s.a.w. Kwa hivyo ni kweli asemavyo mtungaji kuwa Waafrika wanayo haki kudai kuwa dini yao ya asili ni Dini ya Kiislamu. Hakika ni kuwa wanaadamu wote wanayo haki ya kudai hayo. Mwenyezi Mungu Anasema katika aya ya 30 ya Suuratir Rum:
Basi uelekeze uso wako katika dini aliyo sawasawa - ndilo umbile Mweyezi Mungu Alilowaumbia watu; hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini iliyo haki, lakini watu wengi hawajui.
Mwenye kutunga utenzi huu
ni ndugu kwangu kwa mengi. Namjua tangu utoto wake, kwani
baba yake ni mmoja katika mashekhe zangu wakubwa. Marehemu
Sheikh Muhsin alikuwa mwanafunzi mkubwa wa Sheikh Abdulla Baakathir, na ndiye
aliyerithi pahala pake. Mwanawe Sheikh Muhsin, huyu mtungaji,
juu ya kuwa sehemu kubwa ya masomo yake ya dini ameipata kwa baba yake, amesomeshwa
pia na wengine; na miongoni mwao ni mimi. Vile vile kwa miaka
isiyopungua kumi na tano, tulishirikiana katika gazeti mashuhuri la zamani la
Abdulla Saleh Farsy
Kadhi Mkuu wa