1. Naapa kwa mataifa katika viumbe vyangu, walio jipanga
wenyewe kwa safu zilio sawa katika msimamo wa ibada na ut'iifu.
Rudi kwenye Sura
2. Na kwa wanao zuia wanao pindukia mipaka kwa mzuio mkali, nidhamu
ibakie, na ulimwengu uhifadhiwe.
Rudi kwenye Sura
3. Na kwa wenye kusoma Aya, na wanamdhukuru Mwenyezi Mungu kwa dhikri
ya Tasbihi, Kumtakasa, na Kumhimidi, kumsifu.
Rudi kwenye Sura
4. Hakika Mungu wenu anaye faa kuabudiwa bila ya shaka ni Mmoja tu.
Hana mshirika wake, kwa dhati, wala kitendo, wala sifa.
Rudi kwenye Sura
5. Yeye - peke yake - ndiye Muumba mbingu na ardhi na viliomo baina
yao, na ndiye Mwenye kupanga mambo, na ndiye Mwenye kutawala mashariki
za kila chenye mashariki.
Mwenyezi Mungu ndiye Muumba mbingu saba na viliomo baina yao, navyo
ni hivyo vyombo vya mbinguni na nyota zake. Naye ndiye Mwenye kusimamisha,
Mwenye kulinda vile vile juu ya mwahali zinapo chomozea jua na nyota zote.
Na Yeye ndiye anaye vionyesha hivyo kila siku katika pahala huko
upeo wa macho, kila siku pahala mbali na vilipo dhihiri siku iliyo tangulia.
Na hayo ni kwa mwendo wa mpango wa jua maalumu kwa inavyo zunguka dunia
juu ya msumari-kati wake kutoka magharibi kwendea mashariki kila siku na
wakati huo huo inavyo lizunguka jua katika njia yake katika falaki.
Na jua na nyota huonekana na wakaazi wa ardhi kila siku kama zinachomoza
mwahala mbali mbali. Na kila ardhi ikigeuza mahala pake katika safari yake
katika mbingu linaonekana jua linachomoza pahala pengine. Ukiliangalia
jua kwa utulivu kuanzia mwishoni wa mwezi wa Machi, yaani linapo kuwa jua
lipo kati ya mstari wa Ikweta mwanzo wa musimu wa Rabii, yaani Spring,
kwa nusu ya kaskazini ya dunia, utaliona linachomoza pahala katika mashariki
juu ya upeo wa macho. Kwa mwenye kupeleleza kila siku ikipita ataona kuchomoza
kwake kunajongelea kaskazini. Na mwishoni mwa mwezi wa Juni utaona linachomozea
mwisho wa kukaribia kaskazini. Kisha baada ya hapo utaliona jua linarejea
linafuata kugeuka kule kule mpaka mwisho wa Septemba (wakati wa kuwa sawa
wakati wa Khariif yaani Autumn) utaliona jua linachomoza pale pale lilipo
chomoza mwanzo wa Machi. Kisha litaendelea kuelekea kusini kuchomoza kwake
mpaka mwisho wa Desemba linakuwa linachomoza karibu kabisa na kusini. Baada
ya hapo huanza tena kurejea kuelekea kaskazini mpaka limalize safari yake
ya kufika kati sawa katika Rabii ya pili. Na safari hii yote inachukua
siku 365 na robo siku. Na inaonekana kuwa nyota nazo zinachomoza mwahala
mbali mbali katika upeo wa macho inapo kuwa dunia imo katika safari yake
ya mbinguni, na khasa nyota za buruji (au vituo) 12 vinavyo pitiwa na jua
katika mwendo wake wa mwaka.
Rudi kwenye Sura
6. Sisi tumeipamba hii mbingu ya karibu na watu wa duniani kwa mapambo,
nayo ni hizo nyota zinazong'ara, zenye ukubwa mbali mbali, na mwahala pao
mbali mbali kwenye anga la ulimwengu kama ionekanavyo kwa macho.
Rudi kwenye Sura
7. Na tukaihifadhi hiyo mbingu na kila shetani jabari aliye a'si.
Rudi kwenye Sura
8. Hao majabari wa kishetani hawawezi kusikiliza yanayo pita katika
ulimwengu wa Malaika. Na wao hupopolewa kwa kila kinacho faa cha kuwazuia.
Rudi kwenye Sura
9. Hufukuzwa hao kwa nguvu wasifikilie kuweza kusikiliza khabari za
mbinguni. Na Akhera watapata adhabu kali ya kudumu.
Rudi kwenye Sura
10. Isipo kuwa anaye lipata neno moja hivi katika khabari za mbinguni
kwa kuibia. Na huyo naye tunamwandama kwa mwenge wa moto unao murika anga
kwa mwangaza wake, ukamuunguzilia mbali.
Rudi kwenye Sura
11. Ewe Nabii! Hebu waulize hao wanao kanya kufufuliwa wanao ona hayawi
hayo: Je! Kwani kuwaumba wao hawa ni kugumu zaidi au kuziumba mbingu, na
ardhi, na nyota, na vyenginevyo, tulivyo viumba Sisi?
Rudi kwenye Sura
12. Hakika Sisi tumewaumba wao kutokana na udongo unao gandana. Basi
kwa nini wanaona ajabu kurejezwa tena wao?
Rudi kwenye Sura
13. Na wanapo kabiliwa kwa dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu kufufua,
hata hawazishughulikii wakanufaika kwa hizo dalili.
Rudi kwenye Sura
14. Na wanapo ona ushahidi wa kuonyesha uweza wa Mwenyezi Mungu huitana
wapate kupita mipaka katika kumkejeli.
Rudi kwenye Sura
15. Na makafiri husema juu ya Ishara zinazo onyesha uweza wa Mwenyezi
Mungu: Haya tunayo yaona si chochote ila ni uchawi tu.
Rudi kwenye Sura
16. Hivyo sisi tukisha kufa tukawa udongo na mafupa tutatolewa tena
makaburini kwetu tuwe wahai?
Rudi kwenye Sura
17. Sisi tuwe wahai, na pia watafufuliwa baba zetu wa zamani walio
kufa kabla yetu, na wakapotea, na wakateketea?
Rudi kwenye Sura
18. Ewe Nabii! Waambie: Ndio mtafufuliwa nyote, nanyi ni madhalili
na wanyonge.
Rudi kwenye Sura
19. Kwani hakika kufufuliwa ni Ukelele mmoja tu, mara wote watakuwa
wahai wakiyaona waliyo ahidiwa.
Rudi kwenye Sura
20. Na washirikina watasema: Ee msiba wetu huu! Hii ndiyo Siku ya Hisabu
na Malipo kwa a'mali zilio tendwa!
Rudi kwenye Sura
21. Watajibiwa: Hii ndiyo Siku ya Hukumu na kufarikisha vitendo, mliyo
kuwa mkiikadhibisha.
Rudi kwenye Sura
22,23. Enyi Malaika wangu! Wakusanyeni walio jidhulumu nafsi zao kwa
kufuru, pamoja na wake zao wa kikafiri, na miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu
badala ya Mwenyezi Mungu, yakiwa masanamu au watu, na waonyesheni njia
ya kwendea Motoni waingie humo.
Rudi kwenye Sura
24. Na wazuieni hapo hapo; kwani wao hakika watahojiwa juu ya imani
zao na vitendo vyao.
Rudi kwenye Sura
25. Enyi washirikina! Mna nini? Mbona hamsaidiani kama mlivyo kuwa
mkisaidiana nyinyi kwa nyinyi duniani?
Rudi kwenye Sura
26. Leo hii hawasaidiani, bali leo wanaongozwa tu, wamekwisha salimu
amri.
Rudi kwenye Sura
27. Watakuwa wakikabiliana kulaumiana na kusutana, na wakiulizana khabari
za mwisho wao muovu.
Rudi kwenye Sura
28. Wanyonge watawaambia walio jipa ukubwa: Nyinyi mlikuwa mkitujia
upande tulio udhania ni wa kheri na mafanikio, ili mtugeuze njia tuache
Haki twende kwenye upotovu.
Rudi kwenye Sura
29. Watasema walio jipa ukubwa: Sisi hatukukugeuzeni njia, lakini nyinyi
wenyewe mliikataa Imani, na mkaipuuza kwa khiari yenu.
Rudi kwenye Sura
30. Na sisi hatukuwa na madaraka juu yenu hata tuweze kukunyang'anyeni
uweza wenu wa kukhiari. Bali nyinyi wenyewe mlikuwa watu mlio iacha Haki.
Rudi kwenye Sura
31. Basi neno la Mola wetu Mlezi limethibiti juu yetu. Hakika hapana
shaka sisi tutaionja adhabu ya Siku ya Kiyama.
Rudi kwenye Sura
32. Tukakuiteni kwenye maasi na upotovu na nyinyi mkaitikia wito wetu.
Kazi yetu ni kufanya hila ya kuwaita watu wafuate upotovu tulio nao. Basi
hatuna lawama.
Rudi kwenye Sura
33. Kwani hakika wafuasi na wenye kufuatwa wote watashiriki pamoja
katika adhabu ya Siku ya Kiyama.
Rudi kwenye Sura
34. Hakika mfano wa adhabu hiyo Sisi tunawapa wale walio fanya makosa
katika Haki ya Mwenyezi Mungu kwa ushirikina na kutenda maasi.
Rudi kwenye Sura
35. Hakika watu hao walikuwa wakiambiwa: La ilaha illa 'Llah, Hapana
mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakakataa kukiri kwa kiburi na majivuno.
Rudi kwenye Sura
36. Na husema: Sisi tuache kuabudu miungu yetu kwa kufuata kauli ya
mtunga mashairi aliye zugwa asiye kuwa na akili?
Rudi kwenye Sura
37. Bali Mtume wao amewaletea Tawhidi, Imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja,
ambayo ndiyo wito wa Mitume wote, naye akasadikisha kwa hivyo wito wa hao
Mitume.
Rudi kwenye Sura
38. Enyi washirikina! Hakika nyinyi hapana shaka mtaionja adhabu kali
ya Akhera.
Rudi kwenye Sura
39. Na hamtapata malipo Akhera ila malipo ya vitendo vyenu vya duniani.
Rudi kwenye Sura
40. Ila waja wangu walio safika; hao hawataionja adhabu kwa sababu
wao ni watu wa Imani na ut'iifu.
Rudi kwenye Sura
41. Hawa watu wa ikhlasi watapata Akhera riziki maalumu kwa Mwenyezi
Mungu.
Rudi kwenye Sura
42. Matunda ya namna mbali mbali. Nao watastareheshwa na kutukuzwa,
Rudi kwenye Sura
43. Katika Bustani zenye neema.
Rudi kwenye Sura
44. Wakikaa humo juu ya viti wakikabiliana.
Rudi kwenye Sura
45. Watawazungukia watoto na chombo chenye kinywaji kilicho toka kwenye
chemchem zisio katika.
Rudi kwenye Sura
46. Kinywaji chenyewe ni cheupe kinapo changanywa, na kitamu kwa wenye
kukinywa.
Rudi kwenye Sura
47. Hakiwaumizi kichwa na kuwaletea ghururi, wala kwa kukinywa hicho
haiwapotei akili yao kidogo kidogo, yaani hakileweshi.
Rudi kwenye Sura
48. Na watu hawa wat'iifu walioko Peponi watakuwa nao mahuruleini walio
safi, wema, macho yao hayawatazami ila waume zao tu, basi hawayatafuti
matamanio maovu, jicho la mwema haliangalii ila mema.
Rudi kwenye Sura
49. Hao wanawake wenye macho ya staha ni kama mayai ya mbuni, yaliyo
hifadhiwa na mbawa zake. Basi hayaguswi na mikono, wala hayapati vumbi.
Rudi kwenye Sura
50. Hao watu wema watakuwa wakiingia kuulizana hali, na walikuwaje
duniani?
Rudi kwenye Sura
51. Hapo mmoja wao atasema: Mimi nalikuwa na rafiki katika washirikina,
akijadiliana nami katika mambo ya Dini na yaliyo kuja katika Qur'ani.
Rudi kwenye Sura
52. Akisema: Ati wewe ni katika hao wanao sadiki kuwa kupo kufufuliwa
na kuhisabiwa na kulipwa baada ya kufa?
Rudi kwenye Sura
53. Ati baada ya kwisha teketea, tukawa udongo na mafupa, tutakuja
kuwa hai mara nyengine, tuhisabiwe na tulipwe kwa vitendo tulivyo kwisha
vitenda?
Rudi kwenye Sura
54. Muumini awaambie wenzie alio kaa nao: Enyi watu wa Peponi, mnawaona
watu wa Motoni nipate kumwona rafiki yangu?
Rudi kwenye Sura
55. Jicho lake lipige duru kuelekea Motoni, na huko amwone sahibu yake
wa zamani yuko katikati akiadhibika kwa Moto.
Rudi kwenye Sura
56. Akimwona aseme: Wallahi! Ulikaribia kule duniani kunihilikisha
lau ningeli kufuata katika ukafiri wako na maasiya yako!
Rudi kwenye Sura
57. Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi kwa hidaya yake na kuniwezesha
kwake nikamuamini Mwenyezi Mungu na kufufuka, basi ningeli kuwa mfano wako
wewe katika walio hudhurishwa katika hiyo adhabu.
Rudi kwenye Sura
58,59. Je! Sisi tutakaa milele tukineemeka katika Pepo, wala hatufi
kabisa isipo kuwa kule kufa kwetu mara ya kwanza duniani, na wala hatuadhibiwi
baada ya kwisha ingia Peponi?
Rudi kwenye Sura
60. Hakika haya aliyo tupa Mwenyezi Mungu katika ukarimu wa Peponi
bila ya shaka ndiyo kufuzu kukubwa, na kuvuka kukuu na hiyo adhabu tuliyo
kuwa tunatahadhari nayo tangu duniani.
Rudi kwenye Sura
61. Ili wapate ukarimu wa Akhera kama walio bahatika kuupata Waumini,
basi nawafanye kazi duniani hao wafanyao kazi, ili wapate kama walio pata
wao.
Rudi kwenye Sura
62. Je! Hiyo riziki maalumu iliyo andaliwa kwa sababu ya watu wa Peponi
ni bora, au mti wa Zaqqum ulio andaliwa kwa ajili ya watu wa Motoni?
Rudi kwenye Sura
63. Hakika Sisi tumeujaalia mti huu uwe ni mtihani na adhabu ya Akhera
kwa ajili ya washirikina.
Rudi kwenye Sura
64. Hakika huo ni mti ulioko katikati ya Jahannamu, umekulia huko Motoni,
na umeumbwa kutokana na huko huko.
Rudi kwenye Sura
65. Matunda yake mabaya kuyatazama, yana sura ya kukirihisha, macho
hayapendi kuyatazama, kama vichwa vya mashetani ambavyo kwa hakika watu
hawajaviona, lakini mtu humpitikia tu katika dhana jinsi ya ubaya wake.
Rudi kwenye Sura
66. Na wao watakuwa wanakula matunda ya mti huo, na wajaze matumbo
yao kwayo. Kwani hawanacho kinginecho cha kukila.
Rudi kwenye Sura
67. Kisha washirikina hao juu ya kula mti wa Zaqqum watapewa maji yaliyo
changanywa, yamoto, ya kuwababua nyuso zao, na kukatakata matumbo yao.
Rudi kwenye Sura
68. Tena mwisho wao ni Motoni. Wao watakuwa katika adhabu ya milele.
Wataletwa kutoka Motoni waje kula mti wa Zaqqum kisha wanyweshe kinywaji
hicho, na tena warejeshwe mahala pao katika Jahannamu.
Rudi kwenye Sura
69,70. Wao waliwakuta baba zao wamepotoka, na wao wakafanya haraka
kufuata zile zile nyayo za baba zao. Wakawa mbioni kwendea njia yao, wakifuata
tu wala hawachungui, kama walio timuliwa na wakihimizwa wende mbio mbio
kuwafuata hao baba zao bila ya kupima wala kuzingatia.
Rudi kwenye Sura
71. Na hakika walipotea njia ya sawa na njia ya Imani wengi katika
mataifa yaliyo kwisha tangulia kabla ya hawa washirikina wa Makka.
Rudi kwenye Sura
72. Na bila ya shaka Sisi tuliyatumia Mitume hayo mataifa yaliyo tangulia
ili wawaonye na wawahadharishe na adhabu ya Mwenyezi Mungu, nao wakawakadhibisha.
Rudi kwenye Sura
73. Basi angalia, ewe uliye jaaliwa kuangalia, ulikuwaje mwisho wa
walio onywa na Mitume? Bila ya shaka waliteketezwa, wakawa ni mazingatio
kwa watu.
Rudi kwenye Sura
74. Lakini walikuwapo Waumini ambao aliwakhitari Mwenyezi Mungu wamuabudu
Yeye, ili wapate fadhila za ukarimu wake. Basi hao walizipata thawabu zake,
na wakaepukana na adhabu yake.
Rudi kwenye Sura
75. Na hakika Nuhu alitwita alipo kwisha kata tamaa na watu wake, basi
na Sisi tukawa ni wabora wa kuitikia wito wake, tulipo muitikia ombi lake,
na tukawaangamiza watu wake kwa tofani.
Rudi kwenye Sura
76. Na tukamwokoa Nuhu na walio amini pamoja naye, wasizame na kuteketea
kwa tofani.
Rudi kwenye Sura
77. Tukawajaalia vizazi vya Nuhu ndio walio bakia katika ardhi baada
ya kuteketea watu wake.
Rudi kwenye Sura
78. Na tukamwachilia Nuhu kutajwa kwa wema na watu walio kuja baada
yake wakimdhukuru mpaka Siku ya Kiyama.
Rudi kwenye Sura
79. Maamkio ya Salama na Amani kumuamkia Nuhu kutokana na Malaika,
na watu, na majini.
Rudi kwenye Sura
80. Hakika Sisi huwalipa walio tenda mema mfano wa haya. Basi aliingia
katika Jihadi kulinyanyua Neno letu, na akavumilia maudhi kwa ajili yetu.
Rudi kwenye Sura
81. Hakika yeye ni miongoni mwa waja wetu walio tuamini, na wakatimiza
ahadi yetu, na wakaufikisha Ujumbe wetu.
Rudi kwenye Sura
82. Kisha tukawazamisha wenginewe katika makafiri wa kaumu yake.
Rudi kwenye Sura
83. Na hakika bila ya shaka Ibrahim alikuwa akifuata ile ile njia yake
na mwenendo wake katika kuitia Tawhidi, Imani ya Mwenyezi Mungu Mmmoja,
na kumuamini Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura
84. Alipo mkabili Mola wake Mlezi kwa moyo ulio kuwa nadhifu hauna
ushirikina, umemsafia ibada Yeye tu.
Rudi kwenye Sura
85. Alipo chukia kuwa baba yake na watu wake wanaabudu masanamu, akawaambia:
Ni nini haya masanamu mnayo yaabudu?
Rudi kwenye Sura
86. Si mnazua uwongo tu ulio wazi kwa haya myatendayo, kwa kuwa mnamuabudu
asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Na si mnataka kuzua uzushi huu bila ya udhuru
wowote ila kupenda kwenu tu?
Rudi kwenye Sura
87. Mnamdhania nini huyo ambaye ndiye Mwenye haki ya kuabudiwa kwa
kuwa Yeye ndiye Muumba walimwengu wote, mtapo kutana naye na hali nyinyi
mmemfanyia washirika wenginewe katika ibada?
Rudi kwenye Sura
88. Basi akazitupia jicho nyota kuzitazama ili apate kuona dalili ya
Muumba ulimwengu. Akaziona zinageuka, zinabadilika.
Rudi kwenye Sura
89. Akajikhofia nafsi yake asiwe ana upotovu na maradhi ya itikadi.
Rudi kwenye Sura
90. Watu wake wakamwachilia mbali, na wakapuuza maneno yake.
Rudi kwenye Sura
91. Akayaendea kwa haraka yale masanamu kwa kificho, na akayapa chakula
ambacho wale washirikina walikiweka mbele yao ili nao wapate baraka yao
kwa mujibu wa madai yao. Akasema kwa maskhara na kejeli: Mbona hamli?
Rudi kwenye Sura
92. Mna nini hata mmeshindwa kusema lolote, hata ndio au sio?
Rudi kwenye Sura
93. Akayaingilia yale masanamu kuyapiga kwa mkono wa kulia, kwa kuwa
ndio wenye nguvu, akayabomoa.
Rudi kwenye Sura
94. Walipo baini kwamba kuvunjwa miungu yao ni kwa kitendo cha Ibrahim,
basi walimkimbilia ili wamtese kwa alivyo watendea miungu yao.
Rudi kwenye Sura
95. Ibrahim akawaambia kwa kuwahizi: Hivyo nyinyi mnaabudu mawe mliyo
yachonga nyinyi wenyewe kwa mikono yenu? Akili zenu zimekwenda wapi?
Rudi kwenye Sura
96. Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, na akayaumba hata hayo
masanamu mnayo yaunda kwa mikono yenu. Basi Yeye peke yake ndiye Mwenye
kustahiki kuabudiwa.
Rudi kwenye Sura
97. Hoja ilipo wapata wale wanao abudu masanamu, wakaona hawana ila
waingie kutumia nguvu; wakaazimia kumchoma moto. Basi waliambizana:
Mjengeeni jengo, na mlijaze moto, na mtupeni katikati yake!
Rudi kwenye Sura
98. Kwa haya walikusudia kumteketeza, lakini Mwenyezi Mungu alimwokoa
na ule moto baada ya wao kwisha mtumbukiza humo. Hadhi yake ikawa juu kwa
utukufu ule, na Mwenyezi Mungu akawafanya wao ndio watu wa chini.
Rudi kwenye Sura
99. Ibrahim alipo kata tamaa nao, kuwa hawaamini tena, alisema: Mimi
ninahama kwendea pahala alipo niamrisha Mola wangu Mlezi nende. Mola wangu
Mlezi atanihidi aniongoze mpaka nifike pahala pa utulivu, penye amani,
na nchi nzuri.
Rudi kwenye Sura
100. Ewe Mola wangu Mlezi! Nipe dhuriya walio wema wa vitendo, wasimamie
hii kazi ya wito kuwaitia watu kwako Wewe, baada yangu.
Rudi kwenye Sura
101. Malaika wakampa bishara ya kwamba atapata mwana atakaye pambwa
kwa akili na upole.
Rudi kwenye Sura
102. Akazaliwa huyo mwana, na alipo kuwa kijana wa kwenda naye baba
yake katika kutafuta haja za maisha, Ibrahim alipewa mtihani kwa ndoto
aliyo iota. Ibrahim akasema: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini
ufunuo kutokana na Mwenyezi Mungu ananitaka nikuchinje! Basi wewe tazama
unaonaje? Yule mwana mwema alisema: Ewe baba yangu! Tekeleza amri ya Mola
wako Mlezi. Utaniona mimi katika wanao subiri, Inshallah!
Rudi kwenye Sura
103. Yule baba na mwanawe walipo iridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu,
na akamweka juu ya fungu la mchanga na akamlaza juu yake, kipaji chake
kikawa juu ya ardhi, akawa tayari kumchinja.
Rudi kwenye Sura
104,105. Na Mwenyezi Mungu akajua umadhubuti wa Ibrahim na mwanawe
katika majaribio, Mwenyezi Mungu alimwita Ibrahim kwa wito wa kirafiki:
Ewe Ibrahim! Hakika umeuitikia kwa utulivu huo ufunuo wa ndoto, na wala
hukusitasita katika kufuata amri. Basi haya yanakutosha. Sisi tunakupunguzia
haya majaribio yetu kuwa ni malipo kwa wema wako, kama tunavyo walipa walio
wema kwa wema wao.
Rudi kwenye Sura
106. Hakika majaribio haya tuliyo mjaribia Ibrahim na mwanawe bila
ya shaka ni majaribio yaliyo dhihirisha undani wa Imani yao na yakini yao
kwa Mola Mlezi wa walimwengu.
Rudi kwenye Sura
107. Na tukamkomboa kwa mhanga wenye cheo kikubwa, kwa kuwa hayo ni
kwa amri ya Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura
108. Na tukaacha atajike kwa sifa nzuri katika ndimi za walio kuja
baada yake.
Rudi kwenye Sura
109. Maamkio ya amani na salama kwa Ibrahim!
Rudi kwenye Sura
110. Mfano wa malipo kama haya ya kuwakinga na balaa ndivyo tunavyo
walipa walio wema katika kufuata amri za Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura
111. Hakika Ibrahim ni katika waja wetu wanao ifuata Haki.
Rudi kwenye Sura
112. Na kwa amri yetu, Malaika walimbashiria kuwa ataruzukiwa mwana,
Is-haqa juu ya kukata tamaa na kuwa mkewe ni tasa. Na kwamba yeye hakika
atakuwa Nabii miongoni mwa walio wema.
Rudi kwenye Sura
113. Nasi tukamtunukia yeye na mwanawe baraka na kheri duniani na Akhera.
Na miongoni mwa vizazi vyao watatokea watakao jifanyia wema nafsi zao kwa
Imani na ut'iifu, na watakao jidhulumu kwa upotovu wa ukafiri na maasi.
Rudi kwenye Sura
114. Na bila ya shaka tuliwaneemesha Musa na Haruni kwa kuwapa Unabii
na neema kubwa kubwa.
Rudi kwenye Sura
115. Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa iliyo kuwa
iwashukie kutokana na Firauni na kaumu yake.
Rudi kwenye Sura
116. Na Sisi tukawanusuru na adui zao, wakawa wao ndio wenye kushinda.
Rudi kwenye Sura
117. Na tukampa Musa na Haruni Kitabu kilicho wazi chenye kubainisha
hukumu za Dini, nacho ni Taurati.
Rudi kwenye Sura
118. Na tukawaongoza waifuate Njia iliyo sawa.
Rudi kwenye Sura
119. Na tukabakisha sifa njema za kutajika wote wawili hao kwa watu
wengineo walio kuja baada yao.
Rudi kwenye Sura
120. Maamkio ya Amani na Salama kwa Musa na Haruni.
Rudi kwenye Sura
121. Hakika mfano wa malipo tuliyo mjazi Musa na Haruni ndivyo tunavyo
wajazi wote walio wema.
Rudi kwenye Sura
122. Hakika wawili hao ni katika waja wetu wenye kuifuata Haki.
Rudi kwenye Sura
123. Na hakika Ilyas ni katika hao tulio watuma kwenda waongoa watu
wao.
Rudi kwenye Sura
124. Ilyas alipo waambia watu wake, nao walikuwa wakiyaabudu masanamu
yao: Je! Mnaendelea juu ya makosa yenu, na wala hamumkhofu Mwenyezi Mungu
mkajikinga na adhabu yake?
Rudi kwenye Sura
125. Mnaliabudu sanamu linalo itwa Baa'li, na mkaacha kumuabudu Mwenyezi
Mungu aliye uumba ulimwengu na akaufanya mzuri uumbaji wake?
Rudi kwenye Sura
126. Mwenyezi Mungu amekuumbeni na amekuhifadhini nyinyi na baba zenu
wa zamani. Yeye basi ndiye Mwenye haki ya kuabudiwa.
Rudi kwenye Sura
127. Lakini walimkadhibisha, basi jaza yao ni kuhudhurishwa kwenye
Moto Siku ya Kiyama.
Rudi kwenye Sura
128. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safisha Imani yao. Hao
basi ndio wenye kufuzu.
Rudi kwenye Sura
129. Na tukamjaalia awe anatajwa kwa wema na ndimi za walio kuja baada
yake.
Rudi kwenye Sura
130. Salamu juu ya Ilyasi, au juu yake yeye na watu wake, kwa kuwa
kawashinda.
Rudi kwenye Sura
131. Hakika mfano wa malipo tuliyo mlipa Ilyas tunamlipa kila aliye
mwema kwa sababu ya wema wake.
Rudi kwenye Sura
132. Hakika Ilyas ni katika waja wetu walio amini.
Rudi kwenye Sura
133. Na hakika Lut'i ni katika Mitume tulio watuma ili afikishe Ujumbe
wetu kwa watu.
Rudi kwenye Sura
134. Kwa hakika Sisi tumemwokoa yeye na ahali zake wote kutokana na
adhabu iliyo wasibu watu wake.
Rudi kwenye Sura
135. Ila mkewe mkongwe. Yeye bila ya shaka aliteketea pamoja na walio
teketea.
Rudi kwenye Sura
136. Kisha tukawaangamiza wote isipo kuwa Lut'i na walio muamini.
Rudi kwenye Sura
137,138. Na hakika nyinyi, watu wa Makka, mnayapitia majumba ya hao
kaumu Lut'i katika safari zenu za kwendea Sham asubuhi au usiku. Je!
Mmepotelewa na akili zenu hata hamwezi kuzingatia yaliyo wapitia hao kuwa
ni malipo ya ukanushaji wao?
Rudi kwenye Sura
139. Na hakika Yunus ni miongoni mwa tulio watuma wawafikishie Ujumbe
wetu watu.
Rudi kwenye Sura
140,141. Alipo wahama watu wake bila ya amri ya Mola wake Mlezi, akaliendea
jahazi ambalo lilio kwisha sheheni pomoni, akalipanda. Jahazi likapatikana
na mambo ikawajibikia lazima mmoja katika abiria atoswe kupunguza shehena
yake. Kura ikamuangukia Yunus, akashindwa kwa kura. Akatoswa baharini kwa
mujibu wa ada yao zama zile.
Rudi kwenye Sura
142. Samaki akammeza, naye hakika alistahiki lawama kwa kuikimbia kazi
yake ya Daa'wa, Wito, kuwaitia watu wafuate Haki, na kuacha kuwasubiria
wale walio kwenda kinyume naye..
Rudi kwenye Sura
143,144. Na lau kuwa Yunus hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,
wanao dumu kumdhukuru, angeli kufa ndani ya samaki, wala asingeli toka
humo mpaka siku ya kufufuliwa.
Rudi kwenye Sura
145. Tukamtupa pahali patupu kwenye nchi pasipo kuwa na miti wala majumba,
naye ni mgonjwa kwa yaliyo mpata.
Yaliyo mtokea Sayyidna Yunus a.s. ni muujiza. Lakini nayo si muhali
kutokea mtu kumezwa na samaki, na akabakia yuhai ndani yake kwa muda fulani.
Mawili yaweza kuwa -
* Kwanza, ni kuwa huyo samaki ni namna asiye kuwa na meno katika
kabila ya nyangumi wakubwa kabisa, kama nyangumi wanao onekana sana katika
Bahari ya Kati (Mediterranean). Urefu wake huweza kufika Mita 20. Alibaki
Yunus katika mpandikizi wa kinywa chake huyo nyangumi mpaka alipo mtema
kwenye ufukwe mtupu, kwani koo ya nyangumi ni nyembamba hawezi kupita mtu.
* Pili, yaweza kuwa huyo samaki ni namna ya wenye meno pia, kama
nyangumi wa ambari, na ambaye pia urefu wake hufika mita 20. Hawa mara
kadhaa wa kadhaa huonekana katika Bahari ya Kati. Nyangumi hao yawezekana
kwa kawaida kuwameza wanyama wakubwa wanao pita urefu wa mita tatu.
Rudi kwenye Sura
146. Tukauotesha mmea wa kutambaa, usio simama juu ya kigogo, ukamfunika
na kumkinga na madhara ya hali ya hewa.
Rudi kwenye Sura
147. Hata alipo pata nafuu kutokana na yaliyo msibu, tukamtuma awaendee
watu wengi. Wanasema walio waona kuwa wanapata laki moja au zaidi.
Rudi kwenye Sura
148. Wakauwitikia wito wake, nasi tukawakunjulia neema zetu kwa muda
maalumu.
Rudi kwenye Sura
149. Ewe Nabii! Waulize watu wako: Ati Mwenyezi Mungu aliye kuumba
ana watoto wa kike kinyume na wao; na wao ndio wana watoto wanaume
kinyuma na Yeye?
Rudi kwenye Sura
150. Ati tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao hao makafiri waliona
kwa macho yao kuumba kwao, na ndio wakasimulia walio yaona?
Rudi kwenye Sura
151,152. Ewe mwenye kusikia! Yazingatie maneno yao. Hakika wao kwa
uwongo wao wanasema: Mwenyezi Mungu amezaa! Na hali Yeye ametakasika na
upungufu kama huo wa kuwa mzazi au kuzaliwa. Na hakika bila ya shaka hao
ni waongo kwa usemi huo, kwa ushahidi wa dalili nyingi za Upweke wake.
Rudi kwenye Sura
153. Ati Yeye amejichagulia mwenyewe mabinti ambao kwa madai yenu ndio
mnawachukia kuliko watoto wa kiume ambao mnawapenda, na hali Yeye ndiye
Mwenye kuwaumba wote, watoto wa kike na wa kiume?
Rudi kwenye Sura
154. Ni nini lilio kusibuni hata mkakata hukumu bila ya ushahidi? Vipi
mnahukumu hivyo na hali ni upotovu ulio wazi?
Rudi kwenye Sura
155. Je! Mmesahau dalili za uweza wake na kutakasika kwake, ndio msikumbuke
mpaka mkaingia katika upotovu?
Rudi kwenye Sura
156. Hebu nyinyi mnazo nguvu za ushahidi wa kubainisha wa kuthibitisha
hayo mnayo yadai?
Rudi kwenye Sura
157. Basi leteni hoja zenu, ikiwa mnazo hoja za katika Kitabu cha mbinguni,
kama nyinyi ni wakweli katika hayo myasemayo na mnayo yahukumia.
Rudi kwenye Sura
158. Wakashikilia katika itikadi zao, na wakazua baina ya Mwenyezi
Mungu na majini, ambao hawawaoni, kuwa ati yapo makhusiano ya nasaba.
Na bila ya shaka hao majini walikwisha jua kuwa makafiri watahudhurishwa
mbele ya Mwenyezi Mungu ili wapate malipo yao yasiyo kimbilika.
Rudi kwenye Sura
159. Mwenyezi Mungu Mtukufu ametakasika na hizo sifa za kuemewa na
za upungufu wanazo mzulia kuwa anazo.
Rudi kwenye Sura
160. Lakini waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa wakasafishwa
hawana makosa ya huo uzushi wa makafiri.
Rudi kwenye Sura
161,162,163. Enyi makafiri! Hakika nyinyi, na hao mnao waabudu badala
ya Mwenyezi Mungu - Nyinyi kwa kuwaabudu kwenu badala yake Yeye, hamtampoteza
yeyote kwa upotovu wenu. Isipo kuwa yule ambaye tangu hapo Mwenyezi Mungu
Mtukufu anamjua ni katika watu wa Motoni, na huko ataingia.
Rudi kwenye Sura
164. Na Malaika kuwania kuwa wao ni waja wa Mwenyezi Mungu, wakasema:
Hapana yeyote katika sisi ila ana cheo chake maalumu katika ujuzi, na ibada,
na wala hakikiuki hicho.
Rudi kwenye Sura
165. Na sisi tumejipanga safu wenyewe katika misimamo ya kutumika daima.
Rudi kwenye Sura
166. Na hakika sisi bila ya shaka yoyote ndio wenye kumtakasa Mwenyezi
Mungu na kila lisilo kuwa na maelekeo naye katika kila hali.
Rudi kwenye Sura
167,168,169. Na walikuwapo makafiri wa Makka kabla ya kuteuliwa Mtume
s.a.w. ambao wakisema: Lau kuwa sisi tungeli kuwa na Kitabu kama Vitabu
vya watu wa zamani, yaani kama Taurati na Injili, nasi bila ya shaka tungeli
kuwa waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumsafia ibada Yeye.
Rudi kwenye Sura
170. Na Kitabu kikawajia, nao wakakikataa. Basi watakuja jua nini matokeo
ya kukataa kwao.
Rudi kwenye Sura
171,172. Ninaapa! Hukumu yetu kwa Mitume tulio watuma imekwisha tolewa
mbele, ya kwamba ushindi na matokeo mema ni yao wao dhidi ya makafiri.
Rudi kwenye Sura
173. Na kwamba wafuasi wetu na wasaidizi wetu ndio peke yao watakao
washinda walio kengeuka.
Rudi kwenye Sura
174. Basi waachilie mbali, nawe ngoja mpaka wakati ujao. Kwani Sisi
tutakupa wewe matokeo mema, na manusura, na ushindi.
Rudi kwenye Sura
175. Nawe watazame, na uangalie vyema adhabu gani na mateso yatakayo
wapata kwa kwenda kinyume nawe na kukukadhibisha. Basi watakuja ona kwa
macho yao zitakavyo shindwa safu zao, na wataona nusura ya Mwenyezi Mungu
inavyo wafikia Waumini.
Rudi kwenye Sura
176. Je! Wamepoteza akili zao nini, hata wakawa wanaihimiza adhabu
yetu?
Rudi kwenye Sura
177. Basi adhabu hiyo itakapo teremka kwenye uwanja wao mpana, itakuwa
asubuhi ovu kweli hiyo kwa hao walio onywa na adhabu.
Rudi kwenye Sura
178. Na waachilie mbali mpaka mambo yatakapo waishia.
Rudi kwenye Sura
179. Na yaangalie yatakayo wafika wao na yatakayo kufika wewe. Wao
watakuja yaona hayo wanayo yahimiza.
Rudi kwenye Sura
180. Mwenyezi Mungu, aliye kuumba wewe na aliye ziumba nguvu na ushindi,
ametakasika na huo uzushi wanao muambatisha naye.
Rudi kwenye Sura
181. Na salamu zishuke juu ya Mitume wapenzi walio safika.
Rudi kwenye Sura
182. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu peke yake, Muumba wa viumbe
vyote, na Mwenye kuwaangalia makhaluku wote.
Rudi kwenye Sura