1. Ya-Sin: Hizi ni harufi mbili zilizo anzia Sura hii
kwa mujibu wa mpango wa Qur'ani katika kuanzia baadhi ya Sura kwa harufi
moja moja.
Rudi kwenye Sura
2. Ninaapa kwa Qur'ani yenye kukusanya hikima na ilimu yenye manufaa.
Rudi kwenye Sura
3. Hakika wewe, Muhammad, ni katika wale ambao Mwenyezi Mungu amewatuma
kwa watu wawapelekee Uwongofu na Dini ya Haki.
Rudi kwenye Sura
4. Juu ya Njia Iliyo Sawa, nayo ndiyo Dini ya Kiislamu.
Rudi kwenye Sura
5. Ni mteremsho wa Mwenye nguvu Mwenye kushinda kila kitu, ambaye
hapana mtu awezae kumzuia chochote akitakacho. Mwenye kuwarehemu waja wake,
kwa kuwatumia watu wa kuwaongoza njia ya kuokoka.
Rudi kwenye Sura
6. Ili uwaonye watu ambao baba zao wa karibu hawakupata kuonywa,
na kwa hivyo wamesahau yanayo wajibikia kwa Mwenyezi Mungu, na kwa nafsi
zao, na kwa watu.
Rudi kwenye Sura
7. Sisi tulikwisha jua kuwa wengi wao hawatakhiari Imani. Basi yale
tuliyo kuwa tunayajua yamewafikiana na yaliyo kwao. Basi haitakuwapo Imani
kutoka kwao.
Rudi kwenye Sura
8. Sisi tumewafanya hao wanao kakamia juu ya ukafiri ni kama walio
tiwa minyororo shingoni mwao, ikawafika videvuni mwao. Na mikono yao ikawa
imefungwa kwenye vichwa vyao, vikawa vimenyanyuka juu na macho yao yameinama.
Basi hawawezi kuvizungusha vichwa vyao wapate kuona.
Rudi kwenye Sura
9. Na tumewafanya wale walio zuwiwa wasione Ishara na dalili ni kama
walio fungwa baina ya kuta mbili, na macho yao yakagubikwa, wasione yaliyo
mbele yao wala yaliyo nyuma yao.
Rudi kwenye Sura
10. Na ni sawa kwao ukiwahadharisha au ukito wahadharisha, hawaamini
hao.
Rudi kwenye Sura
11. Hakika wanao nafiika kwa kuhadharisha kwako ni wale wanao ifuata
Qur'ani na wakamkhofu Arrahman, ijapo kuwa hawamwoni. Basi watu hawa wape
bishara njema kuwa Mwenyezi Mungu atawasamehe madhambi yao, na atawalipa
malipo mema kwa vitendo vyao.
Rudi kwenye Sura
12. Hakika Sisi tunawahuisha maiti, na tunayaandika yote waliyo yatenda
na wakayakadimisha duniani, na walio yabakisha humo kuwa ni athari, mabaki,
yao baada ya kufa kwao. Na kila kitu kimo katika Kitabu kilicho wazi.
Rudi kwenye Sura
13. Ewe Nabii! Watajie watu wako kisa cha mji mmoja.(1)
Kwani hicho ni kama kisa chao. Waliwaendea Wajumbe walio tumwa ili wawahidi.
(1) Baadhi wa wafasiri wanasema mji huo ni Antiokia.
Rudi kwenye Sura
14. Tuliwatuma wajumbe wawili, wakawakadhibisha. Tukawaongeza nguvu
kwa kumpeleka mwengine wa tatu. Basi hawa watatu wakasema: Hakika sisi
tumetumwa kwenu!
Rudi kwenye Sura
15. Wale watu wa mji wakasema kuwajibu: Nyinyi si chochote ila ni
wanaadamu kama sisi. Na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema hakuteremsha wahyi
wowote kwa mwanaadamu. Nyinyi ni watu mnao sema yasiyo kuwapo.
Rudi kwenye Sura
16. Wale Wajumbe wakasema: Mola wetu Mlezi aliye tutuma anajua
kuwa hakika sisi bila ya shaka tumetumwa kwenu.
Rudi kwenye Sura
17. Na sisi hatuna waajibu wowote ila kufikilisha ujumbe wa Mwenyezi
Mungu ufike kwa uwazi.
Rudi kwenye Sura
18. Wana mji wale wakasema: Sisi tunaona kuwa nyinyi mnatuletea ukorofi.
Na tunaapa, lau kuwa hamsiti na huo wito wenu hapana shaka tutakupopoeni
kwa mawe, na hapana shaka mtapata kwetu adhabu kali yenye kutia uchungu.
Rudi kwenye Sura
19. Wale Wajumbe wakasema: Ukorofi mnao nyinyi wenyewe, kwa hizo
kufuru zenu. Badala ya kuwaidhika kwa mambo yenye kheri kwenu wenyewe,
mnatutuhumu sisi kuwa ni wakorofi, na mnatutishia kutupa adhabu chungu?
Lakini nyinyi ni watu mlio pindukia mipaka ya Haki na Uadilifu.
Rudi kwenye Sura
20. Akaja mtu kutoka huko mwisho wa mji akiwakimbilia wale wanamji,
akawaambia: Wafuateni hawa walio tumwa kwenu na Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye Sura
21. Wafuateni watu wasio taka kwenu ujira wowote kwa kukunasihini
na kukuongozeni, na hali wao wenyewe wameongoka, na nyinyi mtapata manufaa
kwa kufuata njia ya kheri na mafanikio!
Rudi kwenye Sura
22. Na kitu gani cha kunizuia hata nisimuabudu yule aliye niumba,
na ambaye kwake Yeye, si kwa mwenginewe, ndio mtarejea?
Rudi kwenye Sura
23. Je! Niishike kwa kuiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, miungu mingine
isiyo nifaa kitu kuniombea kwao, pindi Mwenyezi Mungu akinitakia madhara?
Wala hawataniokoa nayo yakinishukia hayo madhara.
Rudi kwenye Sura
24. Basi hakika mimi nikiiabudu miungu mingine badala yake Yeye,
nitakuwa katika upotovu ulio dhaahiri.
Rudi kwenye Sura
25. Hakika mimi ninamsadiki Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni, na ndiye
Mwenye kutawala mambo yenu. Basi nisikilezeni na mnit'ii.
Rudi kwenye Sura
26,27. Kuwa ni malipo ya Imani yake na wito wake kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu, ataambiwa: Ingia Peponi! Naye, hali yuko katika kivuli cha neema
na hishima, atasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua alivyo nighufiria
Mola wangu Mlezi na kunipa hishima, nao wakaamini kama nilivyo amini mimi.
Rudi kwenye Sura
28. Na Sisi hatukawaangamiza kwa kuwapelekea maaskari kutoka mbinguni.
Wala huo sio mtindo wetu kupeleka majeshi tunapo yahiliki mataifa.
Rudi kwenye Sura
29. Kuteketezwa kwao hakukuwa ila ni kwa ukelele mmoja tu tulio wapelekea.
Na mara wao wakawa ni maiti, kama moto ulio zimwa.
Rudi kwenye Sura
30. Ee khasara yao, inayo faa kusikitikiwa! Hatuwapelekei waja wangu
Mtume ila wao huwa wakimfanyia maskhara.
Rudi kwenye Sura
31. Kwani wao hawayazingatii mataifa mengi yaliyo tangulia tuliyo
yahiliki? Hakika hao hawarejei tena kwenye maisha yao ya duniani.
Rudi kwenye Sura
32. Hapana katika mataifa yaliyo tangulia na yajayo ila wote watakusanywa
mbele yetu, nao wamelazimishwa kuhudhuria mbele yetu.
Rudi kwenye Sura
33. Na dalili kwao ya uweza wetu wa kufufua ni kuangalia vipi ardhi
yenye ukame tunavyo ihuisha kwa maji, na kutoa ndani yake nafaka wanazo
zila.
Rudi kwenye Sura
34,35. Na humo tukafanya vitalu na mabustani ya mitende na mizabibu,
na tukapasua humo chemchem ya kumwagia maji kwenye miti yake, na ikatoa
matunda, na wao wakala katika hayo. Na hayo si kazi ya mikono yao. Basi
kwa nini hawatoi haki ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yao kwa kumuamini na
kumshukuru?
Rudi kwenye Sura
36. Wa kutakasika ni Mwenyezi Mungu aliye umba kila kitu kwa mpango
wa ume na uke, katika mimea na katika nafsi zao watu, na katika vitu ambavyo
watu hawavijui.
Hii harufi Min , yaani "Katika" katika Aya hii ni ya kubainisha.
Maana yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ameumba madume na majike katika viumbe
vyake vyote, sawa sawa katika mimea, na wanyama, na wanaadamu na vyenginevyo
ambavyo watu hawavijui na hawavioni.
Rudi kwenye Sura
37. Na Ishara pia ya kuwepo Mwenyezi Mungu na uweza wake, ni huu
usiku ambao tunautoa ndani yake mchana, kama kuivua nguo inayo sitiri.
Mara utaona watu wamo gizani lilio wazunguka kila upande.
Rudi kwenye Sura
38. Na jua linakwenda katika njia yake maalumu. Mwenyezi Mungu amekwisha
kadiria kwa zama na mahala. Huo ndio mpango wake Mwenye kushinda kwa uweza
wake, Mwenye kuvizunguka vitu vyote kwa ujuzi wake.
Rudi kwenye Sura
39. Na mwezi kwa mpango wetu tumeujaalia una vituo vyake. Mwanzo
wa mwezi unakuwa mdogo na mwembamba. Kisha kila usiku unazidi kukua mpaka
unatimia kuwa mbaamwezi. Tena unaingia kupungua vile vile, mpaka ukawa
kama karara la mtende linapo kuwa kongwe limepindana na limekuwa manjano.
Rudi kwenye Sura
40. Haipelekei jua likaacha sharia zake likakutana na mwezi, na likaingia
katika njia zake. Wala usiku hauwi kuushinda mchana ukauzuia usije, bali
vyote viwili hivyo hupeana zamu. Na vyote, jua na mwezi, na vyenginevyo
vyote vinaogelea katika njia zao za mbinguni, wala haviachi njia.
Hakika Aya hizi tukufu zinabainisha ukweli wa ki-ilimu ambao wataalamu
walikuwa hawaujui ila mwanzo wa karne ya kumi na nne ya kuzaliwa Nabii
Isa. Na jua ni moja katika nyota za mbinguni, nalo kama nyota zilizo
baki lina mwendo wake wenyewe. Lakini linakhitalifiana na nyota nyengine
kwa kuwa lipo karibu na dunia, na kwa kuwa lina kundi la sayari na miezi
ya mikia na sayari ndogo ndogo zinazo lifuata daima, na zinat'ii mvuto
wake. Kwa hivyo zinakuwa hizo zinazunguka kwa kufuatana kwa utungo kama
sura ya yai. Na mkusanyo wote huu unakwenda angani pamoja na jua kwa mvuto
wake. Kwa ufupi jua, na ardhi, na mwezi na sayari zote na vyombo vyote
hivyo vinakwenda angani kwa mbio maalumu, na kuelekea jiha maalumu. Na
yaonekana kuwa jua na mkusanyo wote huo wake, na nyota zilizo karibu
nalo zipo katika mkusanyo ulio tanda katika mbingu inayo itwa kwa Kiarabu
Sadiimu almajarrah, au kwa Kiingereza Nebula course. Na imebainika kwa
masomo ya kisasa sehemu zote za hiyo Nebula zinaizunguka kati yake kwa
mbio ya kunasibiana na kinyume cha umbali wake kutoka hapo kati. Pia imeonakana
kuwa jua na ardhi na sayari zake na nyota zilio karibu nayo, vyote hivyo
vinakwenda mbio, na upande maalumu. Mbio zake zinafika kilomita 700 kila
nukta moja. Na kunatimia kuzunguka kwake kukizunguka hicho kituo cha kati
kwa kiasi ya miaka milioni 200 ya muangaza.
Na kiini cha maneno ni kuwa Aya tukufu iliyo taja kuwa jua linakwenda
kwa kiwango chake, hawakujua wataalamu uzuri wake wa ndani mpaka katika
mwanzo wa karne hii. Wala hayamkini jua kuupata mwezi, kwani kila kimojapo
kinakwenda katika njia zake mbali mbali, basi ni muhali kukutana, kama
ilivyo kuwa ni muhali kupitana usiku na mchana. Hayo ingeli takikana ardhi
izunguke juu ya msumari-kati wake kutoka mashariki kwendea magharibi, kinyume
na ilivyo hivi sasa kutoka magharibi kwendea mashariki. Na mwezi katika
kuizunguka kwake ardhi, na ardhi kulizunguka jua, huenda pamoja na mkusanyo
wa nyota unao itwa Manaazil Alqamar au Lunar system. Na katika robo
ya mwanzo na ya mwisho wa mwezi huonekana sura yake kama karara kongwe
au kole lilio kauka, linapo kuwa kongwe na kunyauka.
Rudi kwenye Sura
41. Na Ishara nyengine kwao ni kuwa Sisi tuliwapakia wanaadamu katika
jahazi ilio jaa bidhaa zao na riziki zao.
Rudi kwenye Sura
42. Na tukawaumbia mfano wa hiyo marikebu na vyenginevyo wanavyo
vipanda kadhaalika.
Rudi kwenye Sura
43. Na tukitaka kuwazamisha, tunawazamisha. Na wala hawapati wa kuwaopoa,
wala hawapati wa kuwaokoa wasiangamie.
Rudi kwenye Sura
44. Lakini Sisi hatuwazamishi, kwa sababu ya rehema inayo tokana
nasi, na ili tuwastareheshe kwa muda ulio kwisha kadiriwa.
Rudi kwenye Sura
45. Na wanapo ambiwa: Yaogopeni mfano wa yaliyo wapata mataifa yaliyo
kwisha pita kwa kukadhibisha kwao, na iogopeni adhabu ya Akhera ambayo
itakupateni kwa kushikilia kwenu ukafiri, kwa kutaraji kuwa asaa Mola wenu
Mlezi akakurehemuni mkimcha Yeye, wao hupuuza.
Rudi kwenye Sura
46. Na haiwajii hoja katika hoja za Mola wao Mlezi, yenye kuonyesha
Upweke wa Mwenyezi Mungu na uweza wake, ila wao huipa nyongo, hawaijali.
Rudi kwenye Sura
47. Na wakiambiwa: Wapeni mafakiri kutokana na hicho alicho kuruzukuni
Mwenyezi Mungu, makafiri huwaambia Waumini: Je! Tuwalishe watu ambao Mwenyezi
Mungu Mwenyewe angeli taka angeli walisha? Hivyo inakuwa tunamfanyia inda
Mwenyezi Mungu kwenda kinyume na mapenzi yake! Nyinyi mnao taka tutoe,
si chochote ila mmo katika upofu ulio wazi, hamuioni Haki.
Rudi kwenye Sura
48. Na huwaambia Waumini kwa kuwafanyia kejeli: Lini yatatokea hayo
mlio tuahidi, kama nyinyi mnasema kweli katika mnayo ahidi?
Rudi kwenye Sura
49. Hawangojei ila sauti moja tu, iwamalize kwa ghafla, nao wakizozana
katika mambo ya kidunia, wameghafilika na Akhera.
Rudi kwenye Sura
50. Kwa upesi wa hayo yatakayo wateremkia, hawatowahi kuusia chochote,
wala kurejea kwa ahali zao.
Rudi kwenye Sura
51. Na barugumu litapulizwa kwa mpulizo wa kufufua watu. Mara watu
watatoka makaburini mwao wakikimbilia kwenda kukutana na Mwenyezi Mungu.
Na hilo barugumu, na kupulizwa kwake, ni katika anayo yajua Mwenyezi Mungu
Yeye peke yake.
Rudi kwenye Sura
52. Watasema watakao fufuliwa kutoka makaburini: Balaa gani lilio
tushukia! Nani aliye tuamsha tukauwacha usingizi wetu? Jawabu ya suala
lao itawajia: Hii ndiyo siku ya kufufuliwa aliyo waahidia Arrahaman, Mwingi
wa Rehema, waja wake, na Mitume wakaisemea kweli kwa waliyo yasimulia.
Rudi kwenye Sura
53. Wito wao wa kuwatoa hautakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote
watakusanywa mbele yetu wahudhurishwe ili tuwahisabie.
Rudi kwenye Sura
54. Basi katika hii siku ya leo haipungukiwi nafsi na chochote katika
ujira wake kwa kazi iliyo tenda. Na wala hamtopata isipo kuwa jaza ya mliyo
kuwa mkiyatenda, ikiwa ni kheri au shari.
Rudi kwenye Sura
55. Hakika watu wa Peponi hii leo watakuwa wameshughulika kwa neema
walizo nazo, wakistaajabia na kufurahia.
Rudi kwenye Sura
56. Wao na wake zao wamo katika vivuli vilivyo enea, wameegemea juu
ya viti vilivyo pambwa.
Rudi kwenye Sura
57. Watapata huko Peponi kila namna ya matunda, na kila wakitakacho
watakipata.
Rudi kwenye Sura
58. Wataambiwa: "Salama", kuwa ni kauli iliyo toka kwa Mola
Mlezi Mwenye kurehemu.
Rudi kwenye Sura
59. Na wataambiwa wakosefu siku hii ya leo: Jitengeni mbali na Waumini.
Rudi kwenye Sura
60. Enyi wanaadamu! Sikukuusieni kuwa msimfuate Shetani kwa ut'iifu
kama kwamba ni mungu wa kuabudiwa. Hakika yeye ni adui yenu, aliye dhihirisha
uadui wake.
Rudi kwenye Sura
61. Na nyinyi mniabudu Mimi peke yangu, kwani kuniabudu Mimi tu ndiyo
Njia kuu katika kusimamisha Dini sawa.
Rudi kwenye Sura
62. Na Shetani amewapotoa viumbe wengi kati yenu. Nyinyi mmeghafilika
na hayo. Basi hamkuwa mkifikiri mlipo mt'ii yeye?
Rudi kwenye Sura
63. Wataambiwa: Hii ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa mlipo kuwa
duniani. Ndiyo jaza ya ukafiri wenu.
Rudi kwenye Sura
64. Ingieni! Na hilikini kwa joto lake hii leo kwa ukafiri wenu!
Rudi kwenye Sura
65. Leo vitazibwa vinywa vyao, basi havito tamka kitu. Mikono yao
ndiyo itakayo sema nasi, na miguu yao itatamka kwa kutoa ushahidi juu yao
kwa waliyo kuwa wakiyafanya.
Rudi kwenye Sura
66. Na tungeli taka kuwatia upofu duniani tungeli watia upofu, wakawa
wanaipapasa njia ya kupita wasiweze kuiona. Wataionaje nasi tumewapofoa!
Rudi kwenye Sura
67. Na lau tungeli taka kuzigeuza sura zao tungeli zigeuza zikawa
mbaya, juu ya kuwa wana nguvu na vyeo. Hata wasinge weza kwenda mbele wala
kurudi nyuma, kwa kuwa inge kuwa tumevunja nguvu zao.
Rudi kwenye Sura
68. Na tunaye mfanyia umri wake ukawa mrefu, tunamrudisha, kutoka
nguvu akawa dhaifu. Basi je hawayazingatii haya wakayatia akilini ya uweza
wetu kuyafanya haya, na wao wakajua kuwa dunia ni nyumba ya kupita ina
mwisho wake, na kuwa Akhera ndiyo nyumba ya kubaki na kudumu?
Na tunaye mfanyia umri wake uwe mrefu tunamrejesha awe kinyume na
alivyo kuwa. Yaani baada ya kuwa na nguvu anakuwa dhaifu. Hayo ni kwa kuwa
maisha ya mwanaadamu yanapitia vipindi vitatu, kukua, kutimia kukua; na
ukongwe unaanza kwa kunywea kwa mafigo, ini, Ghudda Ddarqiya au Thyroid
gland, na Pancreas, yaani Dongoronya. Na haya huleta athari katika kudhoofika
mwili wote. Mishipa ya damu nayo huanza kukacha na kunywea, na kwa hivyo
hupunguka damu inayo kwenda katika viungo vyote vya mwili, basi ndio huzidi
udhaifu juu ya udhaifu. Na katika sababu za kukonga ni kuzidi nguvu za
kubomoka kuliko kujengeka katika mwili, yaani Metabolism. Na hayo ni kwa
kuwa Khalaya au Cells, za mwili zote zimo katika hali ya kugeuka, na pia
Khalaya za damu, isipo kuwa Khalaya za ubongo wa kichwani na wa katika
mifupa. Hizo hazigeuki muda wote wa uhai. Ikiwa kiasi ya kuundika upya
ni sawa ya kiasi cha kuharibika, basi hapana madhara yanayo tokea. Lakini
ikiwa kuharibika ni kukubwa kuliko kujengeka katika kiungo chochote basi
hapo hudhihiri madhara kwenye kiungo hicho. Na kwa hivyo kila umri ukiwa
mkubwa kiasi cha kujengeka kinapungua na kinazidi kiasi cha kubomoka kwa
Khalaya, na kunadhihiri kunywea, na kupungua nguvu kote. Na hukhitalifiana
kiasi cha kujengeka kwa mnasaba wa kubomoka kwa kukhitalifiana namna ya
mfumo (Nasiij, Texture). Katika hayo yanayo dhihiri kama ngozi iliyo funika
mwili, na zilio funika paipu za kusaga chakula, na paipu za Ghudad, Glands,
zinachakaa kwa upesi zaidi kila miaka ya binaadamu ikipita. Na hii ni sababu
ya kuonekana upesi alama za kuzeeka.
Rudi kwenye Sura
69. Na Sisi hatukumfunza Mtume kutunga mashairi. Wala haifai hivyo,
kwa kuzingatia pahala pake na cheo chake awe mtungaji mashairi! Hii
Qur'ani iliyo teremka juu yake si chochote ila ni mawaidha, na Kitabu cha
mbinguni kilio wazi. Hakikhusiani kabisa na mashairi.
Rudi kwenye Sura
70. Hii Qur'ani ni kumtia khofu mwenye moyo ulio hai ulio nawirika
kwa akili. Na ipite hukumu ya adhabu kuwashukia wanao ipinga Qur'ani, wenye
kukataa uwongofu wake.
Rudi kwenye Sura
71. Je! Makafiri wameingiwa na upofu hata hawaoni kwamba Sisi tumewaumbia
kutokana na iliyo fanya kudra yetu nyama hoa, wanyama wa mifugo, (1) na
wao wamekuwa wanawamiliki, wanawatumilia kama wapendavyo?
(1) Ngamia, kondoo, mbuzi na ng'ombe.
Rudi kwenye Sura
72. Na hao wanyama tumewafanya wawatumikie. Wengine basi wanawapanda,
na wengine wanawala.
Rudi kwenye Sura
73. Na wanapata kwa hao vitu vya kuwapa manufaa, kama sufi, na manyoya,
na nywele, na ngozi, na mafupa, na vinywaji kutokana na maziwa yao. Je!
Wanasahau neema hizi hata wamekuwa hawamshukuru aliye waneemesha?
Rudi kwenye Sura
74. Na washirikina wamefanya miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu
wakiwaabudu kwa kutaraji kuwa ati watawasaidia.
Rudi kwenye Sura
75. Hiyo miungu ya uwongo haiwezi kuwasaidia kwa lolote Mwenyezi
Mungu akiwatakia madhara. Kwani miungu hiyo haiwezi kunafiisha wala kudhuru.
Bali wao kwa hiyo miungu isiyo weza kitu, ni kama askari walio tayarishwa
kwa ajili ya kuwakhudumia na wa kuwalinda na madhara.
Rudi kwenye Sura
76. Basi yasikuhuzunishe maneno yao kumkhusu Mwenyezi Mungu kwa kumkufuru,
na kukukhusu wewe kwa kukwambia mwongo. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaficha
na wanayo yatangaza. Nasi tutawalipa kwa hayo.
Rudi kwenye Sura
77. Je! Binaadamu anakataa kuwepo Mwenyezi Mungu na uweza wake, na
haoni yeye kwamba Sisi, baada ya kuwa hata hayupo, tulimuumba kutokana
na tone la manii dhalili? Na sasa amekuwa mkali wa kutukhasimu kwa uwazi
kabisa?
Rudi kwenye Sura
78. Tena huyu mpingaji aliye dhaahiri ametupigia mfano ambao kwao
anakanya uweza wetu kufufua mafupa baada ya kuoza na kusagika. Na amesahau
kuwa Sisi tulimuumba yeye, naye hata hakuwepo aslani. Akasema kwa kukanya
na kuona haliwezi kuwa hilo: Ni nani huyo atakaye yafufua mafupa nayo yamekwisha
mung'unyika?
Rudi kwenye Sura
79. Ewe Muhammad! Sema: Atayafufua yule yule aliye yaumba hapo mara
ya kwanza. Kwani aliye anza anao uweza wa kufanya tena. Naye ni Mkubwa
wa kujua kila alicho kiumba. Basi haemewi Yeye na kukusanya vipande vipande
baada ya kutawanyika.
Rudi kwenye Sura
80. Aliye kuumbieni moto kutoka mti mbichi, baada ya kwisha kauka.
Nguvu za jua zinaingia ndani ya mimea kwa wasita wa mwangaza. Khalaya
zenye madda ya kijani katika mimea Chlorophyl ndizo zinafyonza Carbon dioxide
kutokana na hewa, na hii huchanganyika na maji yanayo fonzwa na mimea,
na kufanyika Carbohydrates kwa kuathiriwa na nguvu zinazo tokana na mwangaza
wa jua. Tena hufanyika mbao, kuni, ambazo sehemu kubwa ni muundo
wa kimyaa wa Carbon na Hydrogen na Oxygen. Na kutokana na kuni hizi hufanyika
makaa haya ya miti tuyatumiayo. Ukiyachoma makaa hutoka nguvu zilizo kuwamo
ndani yake kwa ajili ya kupikia, na kwa kazi nyingi nyenginezo. Na makaa
ya mawe si chochote ila ni hiyo hiyo mimea na miti iliyo kuwa na kufanyika
kama ilivyo elezwa, na kisha ikazikika kwa njia fulani na kugeuka baada
ya kupita mamilioni ya miaka kuwa makaa ya mawe, kwa kuathirika na hali
za geology kama joto au mdidimizo au menginewe. Na yapasa kuzingatia kuwa
kutajwa katika Aya hii "mti wa kijani" si bure, bali ni ishara ya hiyo
Chlorophyll ya kijani ambayo ni lazima kwa ajili ya kuimeza Carbon dioxide
katika mimea.
Rudi kwenye Sura
81. Kwani hao wamepotelewa na akili zao hata hawajui kwamba aliye
ziumba mbingu na ardhi, juu ya ukubwa wao, ni Muweza vile vile kurejesha
kuwaumba wanaadamu ambao ni wadogo na hali yao ni dhaifu? Kwani? Yeye ni
Muweza sana, na Yeye ni Mwingi wa kuumba, ambaye ujuzi wake umeenea kila
kitu.
Rudi kwenye Sura
82. Hakika shani yake katika kuumba anapo taka kiwe kitu ni kukiambia
tu: Kuwa! Kikawa, na hutokea hapo hapo!
Rudi kwenye Sura
83. Basi Mtukufu ametakasika na kila kisicho laiki na dhati
yake, yule ambaye katika kudra yake upo Ufalme wa kila kitu, kwa kuumba,
na kupanga, na kuendesha - Kwake Yeye peke yake mtarejeshwa, akuhisabuni
kwa a'mali zenu.
Rudi kwenye Sura