1. Alif, Lam, Raa. Hizi harufi na mfano wake, zinazo
fanya maneno yenu, enyi Waarabu, ndizo hizo hizo zinazo fanya Aya za hichi
Kitabu, ambacho ni muujiza unao waemea watu kuuiga. Muujiza ulio wazi unao
fafanua kwa kila mwenye kutafuta uwongozi ndani yake, na uwongofu. Na kwa
hizi harufi za kutamkika zikasikilizana sauti yake wanazinduliwa watu watanabahi.
Basi wasikilize, ijapo kuwa waliwafikiana kuwa wasisikilize.