1. Hakika, ewe Muhammad, unajua kwa ujuzi usio ingiliwa
na shaka yoyote, alivyo fanya Mola wako Mlezi kuwafanyia wale watu wenye
tembo (ndovu), wakataka kuishambulia Nyumba takatifu ya Al-Kaaba.
2. Unajua ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu amejaalia juhudi
yao kutaka kuibomoa Al-Kaaba ivize na ipotelee mbali. Juhudi yao ikapeperuka,
na wao wasipate makusudio yao.
3. Na Mwenyezi Mungu aliwasalitisha na majeshi ya ndege yaliyo watokea
makundi kwa makundi yakifuatana, na yakawazunguka kila upande.
4. Wakiwatupia mawe kutoka Jahannamu.
5. Akawafanya kama majani ya mimea yaliyo sibiwa yakatilifu.