Sheikh Ali Muhsin aliongoza chama cha "Hizbu" (Zanzibar Nationalist Party) na aliongoza jihadi ya Uhuru wa Zanzibar kutokana na Muingereza. Hapo alikuwa
maarufu kwa jina la "Zaim" yaani Mwongozi. Alifanya kazi ya Waziri wa Ilimu na
Waziri wa Mambo ya Ndani, kesha akawa Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo
ya Nje katika serekali ya kidemokrasia ya Zanzibar kabla ya mapinduzi ya Zanzibar
yalio mwaga damu za watu hata ulimwengu ukashituka hapo January 1964.
Baada ya machafuzi hayo ya Zanzibar, aliwekwa jela kwa muda wa zaidi ya miaka
kumi bila ya kushitakiwa, kwa sibabu ya fikra zake za kisiasa.
Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani ametunga tungo kadha wa kadha za dini. Miongoni mwake ni utenzi wa mashairi
ya Kiswahili wa beti 1300 juu ya maisha ya Mtume (s.a.w.). Pia ametunga kitabu cha Kingereza cha kulinganisha Ukristo na Uiislamu ambacho
kakifasiri mwenyewe Mtungaji kwa Kiswahili.
Hivi sasa Sheikh Ali anaishi Dubai, U.A.E.
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com