(Qur'ani) An Nisaa 4.172
Biblia inahakikisha ukweli huu wa Qur'ani. Mara nyingi tunaona Yesu anatafakhari kujitangaza kuwa yeye ametumwa na Mungu, na mara nyingi anaitwa "mtumishi wa Mungu". Katika Injili ya Yohana mathalan tunasoma:
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.Yohana 17.3-4
Kwa unyenyekevu wa
Matendo 3.26
Matendo 3.13
Matendo 4.29-30
Wagonjwa
wanaponyeshwa, ishara zinaonyeshwa, na maajabu yanatendeka. Nani afanyae
yote haya? Ni kudra na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Jina la Yesu huenda
likatumiwa, lakini ni kama chombo tu, wasila, mwombezi, kwani kama atavyokuwa
yeye ni "mtumishi mtakatifu wa Mungu." Katika Matendo 3.26 na 3.13
hapo juu Paulo aliwaandikia Mayahudi ambao walimkataa mtumishi wa Mungu,
Yesu Kristo, alipowajia na utumishi kutoka kwa Mungu wa babu zao Mayahudi,
Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na Yakobo. Mwenyezi Mungu ni yule yule mmoja,
Mitume ni mbali mbali, lakini utumishi wao ni mmoja. Mayahudi wakawakubali wote
waliotangulia wakamkataa Yesu. Mwenyewe Yesu anawasimanga Mayahudi kama
inavyotueleza Injili ya Yohana:
Yohana 7.28-29
Katika
Injili ya Marko Yesu anasimuliwa alimchukua mtoto akasema:
Marko 9.37
Kama
hayo aliambiwa Mtume Muhammad s.a.w. na Mwenyezi Mungu katika Qur'ani:
(Qur'ani) Al Imran 3.31
Yesu
amesema:
Yohana 4.34
Haya
khasa ndio maana ya neno Uislamu. Uislamu ni kujisalimisha nafsi yako kwenye
mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kutenda apendavyo Mola wako Mlezi. Na hicho
ndicho chakula chake Yesu, kama asemavyo, yaani kama anavyohitaji kula kila siku
ili aishi, kama wanavyohitaji wanaadamu wote, basi hali kadhaalika kuwa daima
anajisalimu mbele ya matakwa ya Mwenyezi Mungu aliyemtuma duniani kuwa ni
Mtume. Tena Yesu amesema:
Yohana 7.16-18
Tunaona
basi kwa ushahidi wake mwenyewe Yesu kuwa fakhari yake ni kunyenyekea kwa
Mwenyezi Mungu wake aliyemuumba na akamtuma kwa Wana wa Israili waliopotea kama
kondoo. Kwa uthibitisho wake mwenyewe yeye ni mtumishi wa haki aliyepewa
Unabii na kufanywa Mtume. Hataki utukufu wake yeye, bali utukufu wa Mungu
wake aliyemtuma na kumpeleka awaongoe watu wafwate njia iliyo nyooka. Katika
Injili ya Mathayo anazidi kufafanua nini wadhifa wake na nini cheo chake mbele
ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wanaadamu wenziwe. Alipowateua wanafunzi
wake kumi na mbili kuwapeleka kuwahubiria Mayahudi alisema:
Mathayo 10.40-41
Yeye
mwenyewe Yesu amesema kuwa yeye ni Mtume, yeye ni Mtumishi, yeye ni
Nabii. Je, nini mawazo ya wale wafwasi wake waliomuamini na wakamwona na
wakaishi naye? Injili zinatwambia:
Yohana 6.14
Mathayo 21.46
Mathayo 21.10-11
Luka 24.13-19
Injili
kwa umoja wao zinathibitisha kuwa watu wake Yesu waliokuwa naye na kumuamini na
wakaona miujiza yake tangu kuzaliwa kwake mpaka mwisho wake walimjua kuwa ni
Nabii wa haki, naye ni mtu, mwanaadamu.
"Hakika huyu ni nabii", anasema Yohana.
"waliwona kuwa nabii", anasema Mathayo.
"Huyu ni yule nabii, Yesu", anasema tena Mathayo.
"Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii", anasema Luka.
Jinsi ya hadhari zake asisingiziwe kuwa anazo au anadai sifa za ungu, Yesu
alikataa hata kuitwa "Mwalimu mwema". Sikiliza masimulizi ya Injili
ya Marko:
Marko 10.17-18
Tafsiri
kubwa kabisa ya Biblia iitwayo The Interpreter's Bible inasema kuwa
kauli hiyo ya Yesu, yaani: "Kwa nini kuniiita mwema? hakuna aliye
mwema ila mmoja, ndiye Mungu", imewatatiza wataalamu wa thiolojia (ilimu
ya Ungu) ya Kikristo wa baadaye. Wameona taabu kuambatisha maneno haya yalio wazi
na imani yao kuwa Yesu ni mungu, na hali hapo dhaahiri yake ni kuwa anakataa
ungu. Kwa hivyo basi kujitoa kimasomaso ikaandikwa katika Injili ya Mathayo
(ambayo iliandikwa baada ya Marko) kwa njia nyengine. Ilivyoandikwa katika
Mathayo ni hivi:
Mathayo 19.16-17
Kila
imani ilipozidi kugeuka maandiko mapya yaliandikwa na kunasibishiwa
Yesu. Kitabu hicho The Interpreter's Bible kinaikataa tafsiri ya kusema kuwa
makusudio ya Yesu yalikuwa ni kusema: Kama unanita mwema, basi unakusudia
kuwa mimi ni Mungu. Hayo siyo. Aliyokusudia Yesu kusema ni kuwa :Sifai kupewa
sifa za Mungu.
Mtaalamu wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri, ameandika katika
kitabu chake The Life of Jesus (Maisha ya Yesu):
Mukhtasari wa yote tuliyokwisha yazungumza, ni kuwa tumepata uthibitisho wa
kutosha kutokana na Biblia kuwa Yesu wa Nazareti ni mwanaadamu, Nabii wa Mungu,
na Mtume wake.
Jee, Mtume huyo katumwa kwa nani?