Katika
hoja zinazotolewa na baadhi ya watu kutaka kuthibitisha ungu wa Yesu ni miujiza
inayosimuliwa kuwa aliitenda. Mifano ya miujiza hiyo ni kugeuza maji yakawa
mvinyo, kuponyesha wakoma na waliopooza, kuwachomoa waliopandwa na pepo,
kufufua waliokwisha kufa, na kutembea kwa miguu juu ya maji. Lakini
hizo hizo Injili zinazosimulia miujiza hiyo zinatwambia vile vile ya kwamba
Yesu mwenyewe alisema kuwa akifanya yote hayo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu
aliyemtuma. Wala si kama Yesu alikiri kuwa miujiza tu ni ya Mwenyezi Mungu,
bali lo lote alilosema au alilolitenda alisema kuwa ni kwa amri, na upendo wa
Mwenyezi Mungu. Yeye hakuweza kuvunja udole bila ya uwezo wa Mola wake. Katika
Injili ya Yohana Yesu anasimuliwa kusema:
Yohana 12.49-50
Yohana 5.30
Fakhari
kubwa ya Yesu ilikuwa kwamba kila alisemalo na alitendalo ni kufuata mapenzi ya
Mungu na kutii maamrisho yake.
Katika hadithi ya muujiza wa kufufuliwa Lazaro tunasoma kama ilivyo katika
Injili ya Yohana:
Yohana 11.38-42
Kutokana na kisa hichi tunajifunza nini? Mambo matatu hapa yanatudhihirikia wazi:
Hayo ndiyo, lakini yeye mwenyewe Yesu kafufuka kutoka wafu.
Huo si muujiza wa kuonyesha kuwa
yeye ni Mungu? Hebu tuitazame Biblia inasema nini juu ya tukio hili. Kila tusomapo
kitabu hichi kitakatifu tunaona kuwa ni Mungu ndiye aliyemfufua Yesu.
Hatuoni kuwa Yesu kajifufua mwenyewe. Vile vile tunasoma humo humo kuwa si yeye
peke yake aliyesimuliwa na kuaminiwa kuwa kafufuliwa kutoka wafu. Twasoma
katika 2 Wafalme:4.32-37 vipi Nabii Elisha (Al Yasaa)
alivyomfufua mtoto aliyekwisha kufa. Kisa kingine kama hicho kinasimuliwa
katika 1 Wafalme 17.22. Biblia pia inawataja watu wengine
wasiokuwa Yesu waliopaa wakenda mbinguni. Katika 2 Wafalme tunasoma:
2 Wafalme 2.11
"Kisulisuli"
ni upepo wa chamchera au kimbunga. Hadithi kama hizo za watu watukufu
kupaa mbinguni na kufufuka zilikuwa zimeenea sana katika zama za Yesu.
Josefas akiandika katika kitabu Antiquities (Ya Kale) anasimulia khabari
ya Musa: "Kwa ghafla kiwingu kilisimama mbele yake, naye akapotea
katika bonde fulani, ijapokuwa ameandika katika vitabu vitakatifu ya kuwa
alikufa. Hayo yalifanywa kwa kuogopa wasije kusema kuwa kwa sababu ya
uchamngu wake uliopita kiasi, alikwenda kwa Mwenyezi Mungu." Josefas
pia ametaja kuwa baadhi ya watu walifikiri kuwa "Musa ameingizwa katika
ungu."
Na J. Jeremias katika Moyses amesema:
"Watatu wamepaa mbinguni nao wahai: Enoko, Musa na Eliya".
Almuradi tunaona kwa uthibitisho wa maandiko matakatifu ya Kikristo kwamba si
Yesu peke yake aliyeitwa "Mwana wa Mungu, au Mungu", wala si yeye
peke yake aliyefufua wafu, wala si yeye peke yake aliyefufuka na kupaa
mbinguni.