Hebu
yazingatie Mahubiri ya Yesu aliyotoa juu ya Mlima wa Zaituni:
Mathayo 5.17-20
Mnamo
mahubiri ya Mlima wa Zaituni ndio yanapatikana mafunzo makubwa ya Yesu
Kristo. Tunaweza kusema kuwa humu, khasa, ndio umo Ukristo; yaani
ikiwa tunaamini ya kuwa Yesu ndiye Katika kifungu cha maneno hayo tuliyoyanukulu
ya Yesu tunaona ya kuwa ni muhali mtu kuingia katika ufalme wa mbinguni, yaani
Peponi, mpaka haki ya mtu izidi ile ya waandishi na Mafarisayo. Yaani wema
uutendao uzidi ule wa wanazuoni wa Kiyahudi. Ni nini hiyo haki ya
waandishi na Mafarisayo? Ni kuifuata sharia ya Taurati neno kwa neno, na
pia waliofunza manabii wengineo. Ndio maana Yesu akasema: "Msidhani
ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, sikuja kutangua, bali kutimiliza."
Kazi yake haikuwa kutengua sharia ya Taurati na kuleta kitu kingine cha
kutengua au kugonganisha na mafunzo ya sharia ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake,
bali kaja yeye kutimiliza kwa kuwafunza Mayahudi umuhimu wa mambo ya kiroho
katika sharia. Kutii madhaahiri ya sharia tu na kuwacha undani wake, uchamngu,
hakutoshi. Mwenyezi Mungu atiiwe kwa dhaahiri na kwa siri. Yesu
alishikilia sana kufundisha na kutenda, aliposema: "Basi mtu ye
yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu
hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali atakayezitenda
na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni."
Katika amri za Taurati ni kama hii iliyomo katika Biblia:
Mambo ya Walawi 11.7-8
Walawi 17.14-15
Hizo ni
amri ziliomo katika Taurati, sharia ya Mungu, ambayo Yesu amesema kama ilivyo
katika Injili ya Mathayo kuwa mwenye kuivunja ndogo yao na akawafundisha watu
hivyo basi ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Na kuvunja
hayo khasa ndio Paulo kafundisha. Msikieni:
1 Wakorintho 10.25-26
Mnamwona
Paulo anavyobomoa sharia ya Taurati waliyoifwata Manabii wote, hata Yesu
na wanafunzi wake thenashara, ya kuwa kuna vyakula vilivyo halali na kuna
vingine ni najisi, haramu kuliwa, kama nguruwe, vya kunyongwa na damu?
Yesu kafunza nini, na Paulo anafunza nini!
Katika waraka wake aliowapelekea Wagalatia Paulo anasema:
Wagalatia 5.4-6
Kwa
kauli moja Paulo ameitengua sharia yote. Yesu kasema nini juu ya Mlima wa
Zaituni na Paulo anasema nini katika barua yake kwa Wagalatia? Yesu
alifuata sharia ya Mwenyezi Mungu na aliihishimu na akaahidi kuwa yeye
hatoitengua kabisa, ila ataitimiza. Paulo anaibeza sharia na kuiona kuwa ni
laana. Yesu akila kilicho halalishwa na Mungu, na alikiepuka kilicho harimishwa
na Mungu. Paulo anatwambia tule kila kiuzwacho sokoni bila ya kujali dhamiri
yetu. Yesu na Manabii wote tangu Nabii Ibrahim walitahiriwa kwa kufuata
amri ya Mungu kama isemavyo Biblia:
Mwanzo 17.9-10
Paulo
mjuaji, anasema kumpinga Mungu:
Wagalatia 6.15
Katika
barua yake aliyowapelekea Warumi ndio kabisa Paulo anaiangamiza sharia ya Mungu
na kufanya vitendo kuwa havina maana yo yote.Chenye maana peke yake ni imani
tu.
Warumi 3.28
Kwa
Paulo kuamini kuwa Yesu kafa msalabani na damu yake kuwa ni fidia kwa dhambi zetu
ndio kwenye maana, sio kufuata sharia wala vitendo. Kwake yeye ile
Taurati, ambayo Yesu mwenyewe hakuja kuitengua bali kaja makusudi kuitimiza, ni
kifungo na pingamizi. Anawaambia Warumi:
Warumi 7.6
Paulo
anaiona Taurati ni kifungo, pingamizi, bali ni laana. Hayo sio maoni ya Yesu
ambaye amesema: "Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta
moja ya torati haitaondoka." Je, kwa kuingia Paulo katika umoja wa
Kikristo ndio tusema mbingu na nchi zimeondoka? Au kwa kutundikwa Yesu
msalabani (ikiwa kweli katundikwa) ndio tuseme mbingu na nchi zimeondoka? Mbona
watu wameyasahau upesi maneno ya Yesu mwenyewe, na kuyasikiliza ya Paulo? Kwa
sababu yanakubaliana na matamanio yao?
Mafunzo ya Paulo yalileta mzozano na ubishi mkubwa tangu pale mwanzo katika
historia ya Kanisa baina ya kikundi chake cha Wakristo waliomfuata kutoka
upagani, na wale Wakristo wa asli ya Kiyahudi. Wao walipinga moja kwa
moja ile shauri ya kwenda kupelekewa mafunzo ya Ukristo mataifa waliokuwa
hawakutahiriwa, wala hawaikubali sharia ya Taurati. Baadhi ya wanafunzi
wa Yesu walikuwa hawakubali hata kula nao wale "wasiotahiriwa".
Wao walikuwa wanajua vyema kuwa Yesu aliwakataza wasend kuwahubiria mataifa
mengine isipokuwa Mayahudi tu, kwani ni wao ndio walikuwa wanaamini Mungu Mmoja
na wao ndio wakiifuata sharia ya Mungu. Mwishoe ulifanywa mkutano na yakawapo
baadhi ya masikilizano kuwa yafaa kuhubiriwa Ukristo kwa mataifa yasiokuwa ya
Kiyahudu, na wao wasilazimishwe kubeba mizigo mizito katika dini kama vile
wenye asli ya Kiyahudi. Walitumwa Paulo na Barnaba kuwaendea hao mataifa,
nao ni Wazungu wa Kirumi na Kigiriki, na wakachukua barua iliomalizikia maneno
haya muhimu:
Matendo 15.28-29
Nyama
zilizosongolewa, yaani nyama za kunyonga, zisiochinjwa. Yazingatieni haya si
maamrisho ya Yesu, lakini ni masikilizano baina akina Paulo na wanafunzi wake
Yesu,(kwa ridhaa ya Roho Mtakatifu) baada ya kuwa Yesu mwenyewe hayupo tena.
Ikiwa hayo ndiyo waliokubaliana ilikuwaje Paulo tena kuwaandikia Wakorintho:
"Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni bila ya kuuliza-uliza, kwa ajili ya
dhamiri"? Lakini Paulo ni Paulo.
Mtakatifu Paulo anadai kuwa yeye aliteuliwa makhsusi kuwa ni mtume wa Yesu
katika ufunuo (Wahyi), na kuwa bado yeye anaendelea kupata amri moja kwa
moja kutokana na mwenyewe Bwana Yesu, ijapokuwa amri hizo na mafunzo hayo
yanapingana kabisa na yale waliyoyapata wale wanafunzi wake Ysu waliokuwa naye
mwenyewe alipokuwa hai. Yeye Paulo hakupata kuonana na Yesu, bali yeye alikuwa
ni mpinzani mkubwa wa Ukristo na akawa ni sababu ya kuteswa na kuuwawa Wakristo
kadhaa wa kadhaa, mmoja wao ni Mtakatifu Stefano, shahidi wa mwanzo katika
Wakristo. Paulo alikuwa na asli ya Kiyahudi, na dini yake rasmi ilikuwa ya
Kiyahudi. Kwa kuwa alizaliwa nje ya Palastina katika mamlaka ya Kirumi
alikuwa na uraia kamili wa Kirumi, na huko alipata fursa ya kusoma ilimu na
falsafa za Kiyunani. Mazingara yake yote ya Kigiriki na Kirumi yalikuwa
ya kikafiri, kipagani. Kwani Magiriki na Warumi walikuwa washirikina
wenye kuamini chungu ya miungu, kama ilivyokuwa ada ya karibu mataifa yote ya
wakati ule isipokuwa Mayahudi. Yalipozuka mafunzo ya Yesu Kristo, ambayo kwa
asli yake hayakuwa ila ni kuendeleza ile ile imani ya Kiyahudi ya Mungu Mmoja
na kufuata sharia ya Taurati na kuongeza uchamngu, na ikawa mafunzo hayo
yanaendelea juu ya kupingwa, Paulo aliona anaweza kuipa nguvu hiyo dini au kwa
hakika madhehebu mpya kwa kuwatia wale Warumi na Magiriki kwa kuchanganya imani
zao na falsafa zao pamoja na imani ya Kiyahudi. Mayahudi wanaamini Mungu
Mmoja, ndio. Ukristo unaamini Mungu Mmoja. Magiriki na Warumi wanaamini
miungu mingi, si chini ya watatu, ndio na Ukristo nao unaamini hivyo. Jee, si
pana mgongano hapo? La, katika Ukristo imani ni ya Mungu Mmoja katika Utatu
Mtakatifu: Mungu Mmoja, mwenye nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Mapagani wa Kigiriki na Kirumi wakiamini mungu aliyekufa, akafufuka na akapaa
mbinguni. Hilo si kitu wanaweza kuendelea na imani hiyo katika Ukristo. Wazungu
magovi hawataki kutahiriwa. Hapana kitu, kutahiriwa si kitu wala kutotahiriwa.
Hoja ipatikane tahara ya roho. Wazungu wamezoea kula kila kitu, nguruwe, damu,
kilichochinjwa na kisichochinjwa. Hilo si tatizo, mtaendelea vivyo hivyo, kwani
dhambi ni kitokacho mdomoni, sio kiingiacho. Kuleni kila kiuzwacho
sokoni. Hapana halali wala haramu. Huo ndio Ukristo mpya wa Paulo, na
hiyo ndio Thiolojia yake ambayo, inasikitisha Wakristo wameifuata, wakayaacha
mafunzo mepesi na yaliyonyooka ya mwenyewe Yesu Kristo.
Hayo ni maji makuu, letu sisi ni kuangalia yaliyomo ndani ya Biblia Takatifu.
Tuiache hiyo iseme. Khabari za kugeuka Paulo akaacha kumpinga Yesu, na
badala yake akawa mfuasi wake zinasimuliwa pahala patatu katika Matendo ya
Mitume katika Agano Jipya la Biblia. Na katika zote mara tatu kisa hicho
kinakhitalifiana katika mambo muhimu. Kwanza tunasoma katika Sura ya 9 mstari
wa 3 mpaka wa 7:
Matendo 9.3-7
Katika
maelezo hayo hapo ni mwandikaji anasimulia. Yapo mambo mane lazima tuyazingatie
vizuri katika maelezo hayo:
Katika
Biblia hiyo hiyo, katika kitabu hicho hicho cha Matendo ya Mitume, sura 22,
mstari wa 6 mpaka wa 10 ipo ncha ya pili ya hadithi kusimulia tukio lile lile.
Msimulizi hapa ni Paulo mwenyewe:
Matendo 22.6-10
Ncha
hii yakubaliana na ile ya mwanzo katika mambo haya:
Ncha
hii lakini inakosana na ile ya kwanza kuwa ya kwanza yasema ya kuwa wale
waliokuwa naye "wakasimama kimya, wakisikia sauti, lakini haikusema kuwa
waliona nuru.
Katika ncha hii ya pili twaambiwa: waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile
sauti.
Ncha ya tatu ya tukio hilo hilo muhimu kabisa katika historia ya Ukristo
inaelezwa katika maneno yake mwenyewe Paulo vile vile kama inavyosimuliwa
katika kitabu kile kile cha Matendo ya Mitume sura ya 26 mstari wa 12 mpaka wa
18:
Matendo 26.12-18
Sasa hapa tunaona khitilafu kubwa na zile ncha za hadithi ziliomo katika sura ya 9 na sura ya 22 katika hicho hicho kitabu kimoja cha Matendo ya Mitume. Hebu tuchungue:
Ni wazi
kuwa Paulo kabla ya kutanasari kwake alikwisha jitayarisha namna gani
atavyougeuza Ukristo wa Yesu, waliokuwa wakiujua wote wanafunzi wake kumi na
mbili, uwe Ukristo wake yeye Paulo.
Na kwa nini Paulo aliongeza mengi aliposimulia mara hii ya tatu kuliko
ilivyosimuliwa zile mara mbili za mwanzo? Ni kwa sababu hapa anasema na
Mfalme Agripa. Lakini yafaa tusite na tujiulize: Nini thamani ya
shahidi anayetoa ushahidi wake kwa polisi, akaubadilisha kidogo akifika kwa
hakimu, na akatoa hadithi nyengine kabisa anapofika mahkama kuu kwa jaji?
Hapana awezae kumueleza Paulo alivyo kama alivyojieleza mwenyewe katika barua
yake aliyowapelekea Wakorintho. Amesema:
1 Wakorintho 9.19-22
Yaweza
kuwa ni kweli kuwa mwenyewe Paulo akiamini kuwa hila hizo zote azitendazo ni
kwa ajili apate "kuwaokoa watu." Wengi miongoni mwa wataalamu
wa Biblia wanakubaliana na Dr. Craveri na Dr. Schonfield kuwa makusudio ya
Paulo ni kuwa apate yeye binafsi wafuasi wengi zaidi ili apate kuwashinda wale
wanafunzi wa Yesu mwenyewe. Kwa hivyo ndio akawa hasikii haoni. Kwa lengo hilo
yu tayari kufanya lo lote, hata akakhiari kugeuza mafunzo ya Kristo ili apate
wafuasi yeye "kwa jina la Kristo." Kwa hakika wale wafuasi wake
kutokana na mataifa walibakia kuwa vile vile makafiri ila waligeuzwa jina tu,
wakaitwa Wakristo. Ndio hivyo alivyowaandikia Warumi:
Warumi 10.8-9
Ndio
hivyo Ukristo umerahisishwa na Paulo ili isiwe taabu kwa makafiri waweze kuitwa
Wakristo bila ya kuufuata Ukristo wa Yesu. Katika mtindo huu Paulo alipata upinzani
kutokana na wengi, kama tunavyoona katika waraka wa Yakobo, nduguye Yesu,
unavyofunza imani ya matendo, si imani tupu. Natusome:
Yakobo 2.14-26
Mafunzo
haya yanapingana moja kwa moja na yale ya Paulo, na yanakubaliana moja kwa moja
na yale ya Yesu, mwenyewe. Si ajabu basi kumsikia Paulo anakakamia kwa
hasira isiyofichikana akisema:
2 Wakorintho 11.12-15
Ni
dhaahiri kuwa Paulo anakusudia kwa matusi yake haya kuwatukana wale wanafunzi
wa Yesu, ambao Yesu mwenyewe aliwateua, ambao wakiongozwa katika kutimiliza
ujumbe wa Yesu na watu kama Yakobo, ambaye anaambiwa kuwa ni nduguye
Yesu. Je, sisi tutendeje tunapokabiliwa na maoni mbali mbali
yanayogongana miongoni mwa watu ambao wote wanadai kuwa ni wanafunzi wa Yesu,
ijapokuwa huyu mmoja Paulo, hata hakumwona Yesu, na huo ushahidi wa kuwa
kamwona katika njozi ni wake yeye tu, tena unagongana na kupingana wenyewe kwa
wenyewe? Tutendeje? Liliopo ni tuyaendee mafunzo yake mwenyewe Yesu,
ambayo ijapokuwa yametatanishwa na maongezo na mapunguzo, lakini hayaachi
kuwepo ya kutosha kwa jumla kutufahamisha nini khasa mafunzo yake. Ikiwa
kweli tunatafuta hakika ya mambo na ukweli wake basi tutayachukua yale yalio
wazi, dhaahiri, katika maneno yake mwenyewe Yesu, na tusiyabali yale ambayo ni
maneno ya wasimulizi. Kadhaalika yasitushughulishe yale ya mafumbo
yanayotatanisha tukajaribu kuleta tafsiri na maelezo tuyapendayo nafsi
zetu. Ikiwa ni kufasiri basi tufasiri fumbo kwa kauli ya Yesu ilio wazi.
Wapotoshaji hufanya kinyume cha hayo.
Mafundisho yaliyotulia kabisa ya Yesu ni yale aliyohubiri juu ya Mlima wa
Zaituni. Na maoni yake yaliyo wazi na kauli ya kukata juu ya sharia na
matendo, ni yaliyomo katika sura 5 ya Mathayo. Akizungumzia juu ya wale
wanaodai kuwa wao ni wafuasi wake, na kuwa ati wanafunza mafunzo yake, na huku
kumbe wanayapotoa yale aliyoyafunza, Yesu anaambiwa kasema:
Mathayo 7.21-27
Hayo ni
maneno aliyokhitimishia Yesu mawaidha yake juu ya Mlima wa Zaituni. Ni
maneno yaliyokaa sawa, yawazi, hayana ubabaishi. Ni nani hao
"watendao maovu", hao wapumbavu, wasiofuata mafunzo ya Yesu
wakayatenda, mafunzo ambayo msingi wake ni kutimiliza sharia na manabii, na
kutenda mapenzi ya Mungu? Ni nani hao wanaodai kufanya miujiza na
kuponyesha watu kwa jina la Yesu, na kudai kuwa ni mitume wa Kristo, na huku
wanapinga mafunzo yake, na kuwaambia watu kuwa wataokoka kwa imani tu kwamba
Yesu kafa msalabini kwa ajili yao, bila ya haja ya vitendo? Ni nani hao
wanaolitumia jina la Yesu naye mwenyewe atawakataa? Kama tuna akili basi
yafaa tuitumie. Tusiwe kama mtu mpumbavu ajengaye nyumba yake juu ya
fungu la mchanga. Tutaanguka, na anguko letu litakuwa kubwa.
Mafunzo ya Yesu Kristo si haba, lakini kwa ufupi wa maisha yake (aliwahi
kuhubiri kiasi miaka miwili mitatu tu) na kutokuwa tayari ulimwengu kuchukua
kweli yote, hakuweza kutimiza ujumbe wote wa Mwenyezi Mungu. Ni hikima
yake Mwenyezi Mungu kuwa kila nabii aliyemleta alikuwa anaongeza juu ya yale
yaliyotangulia. Ni kweli Yesu alisema kama ilivyo katika Mathayo
5.17-20 ambayo tumekwisha yataja kuwa yeye alikuja kutimiza Taurati na
mafunzo ya Manabii, hakuja kutengua lo lote katika hayo. Ulipokaribia
wakati wake wa kuondoka aliungama kuwa mengi aliyo nayo hana nafasi ya
kuyasema, lakini atakuja mwenginewe ambaye atauwongoza ulimwengu kwenye kweli
yote, na ataufundisha ulimwengu mafunzo kaamili juu ya dhambi na haki.
Injili ya Yohana inanukulu maneno ya Yesu:
Yohana 16.5-14
Kwa
mujibu wa maneno hayo kama ilivyo katika Injili ya Yohana, Yesu anawaambia
wanafunzi wake kuwa yeye yu karibu kuondoka duniani, na ya kwamba hajatimiza
ujumbe wake, lakini atakuja mwenginewe ambaye ameitwa majina mbali mbali kwa mujibu
wa tafsiri mbali mbali za Biblia. Hapa anaitwa Msaidizi katika tafsiri
hii ya Kiswahili inayoitwa Union Version. Kwa mujibu wa tafsiri ya
zamani ya Kiingereza, King James's Authorised Version, anaitwa Comforter,
yaani Mliwazi; na kwa mujibu wa tafisiri nyengine ya Kiingereza ya kisasa
Revised Standard Version, anaitwa Counsellor, yaani Mshauri, na
tafsiri nyengine mpya mpya za Kiingereza anaitwa Helper, ambayo maana
yake pia ni Msaidizi. Tafsiri ya Kiarabu ya Darul Kitabul Muqaddas ya
Cairo anaitwa Al Mu'azzi yaani Mliwazi. Vyo vyote vile iwavyo huyo
Msaidizi, au Mliwazi, au Mshauri, ameelezwa na Yesu kwamba:
Hebu
natuichungue bishara hii ya Yesu bila ya chuki, bila ya mapendeleo, na bila kutiwa
pingu na mawazo tuliyofungwa nayo tangu utotoni. Sasa tu watu wazima na
tuna akili zetu, natuzitumie. Wakristo wengi wanachukulia kuwa huyo Msaidizi ni
Roho Mtakatifu, nafsi ya pili ya Mungu. Hivyo ndivyo walivyofundishwa
Kanisani na mapadri. Imani hii yazidi kutiliwa nguvu na hiyo kauli
"huyo roho Mtakatifu" iliotiwa kati baada ya neno
"Msaidizi" liliomo katika mstari wa 26 sura ya 14 ya hii Injili ya
Yohana. Hapana lawama basi kuwa baadhi yetu tukawa tunaamini kuwa Yesu ametwambia
katika Yohana 14 na 16 kuwa atakuja Roho Mtakatifu ndiye atayetuongoza na
kutufundisha yote yaliyobaki sisi kufunzwa, na ambayo yeye Yesu hakuwa na
wakati kufundisha au watu wakati ule walikuwa bado hawajawa tayari
kuyapokea. Kwa kuwa Roho Mtakatifu anaongoza Kanisa la Yesu (yaani ndio
Mapadri, tangu Baba Mtakatifu mpaka Maaskofu na Mapadri wote, na Wazee wa
Kanisa, na Wachungaji) ndio Wakristo hawana wasiwasi wala hawajiulizi kwa
nini leo wanafundishwa mambo ambayo Yesu hakuyafundisha, na wanapewa amri, au
kukatazwa jambo, ambalo Yesu hakuliamrisha au hakulikataza. Roho Mtakatifu ni
Nafsi ya Mungu, ni sawa sawa na Yesu, basi ana madaraka kuendelea kufunza,
kuamrisha na kukataza, kama Yesu, Mungu Mwana, na Mwenyezi Mungu, Mungu
Baba. Yesu alionekana na watu walimwona. Alisema na maneno yake
yameandikwa. Lakini Roho Mtakatifu ananon'gona na Mapadri tu na Wakristo
wanafuata wanayoambiwa na Kanisa, yaani Mapadri. Si ajabu kuona wanaojiita
Wakristo wanafuata Kanisa zaidi kuliko kumfuata Yesu Kristo mwenyewe kwa sababu
wamejazwa katika akili zao kuwa nafsi ya pili ya Mungu ipo Kanisani ikiendeleza
kuugeuza Ukristo wa Yesu kama ipendavyo hiyo nafsi. Lakini natuyazingatie haya:
Kwa mujibu wa imani ya Kanisa, Roho Mtakatifu ni Mungu, ambaye ni sawa na Mungu
Baba, na Mungu Mwana. Tumeona katika maneno ya Yesu kuwa Msaidizi atakuja
baada yake Yesu, yaani wakati huo hakuwako. Je, tuseme kuwa wakati wa Yesu
hakuwako Mungu Roho Mtakatifu? Mbali ya kuwa Roho ameelezwa mara nyingi
sana katika Agano la Kale, na kuwa ndio akiwaongoza manabii wote, bali Wakristo
wanaamini kuwa waandishi wote wa vitabu vya Biblia, kabla na baada ya Yesu,
waliongozwa na Roho Mtakatifu. Tunasoma humu humu katika Injili ya Yohana sura
ya kwanza mstari wa 32:
Yohana 1.32
Tena
tunasoma katika Injili ya Marko:
Marko 1.12
Na
tunaona katika Luka:
Luka 1.15-16
Roho
Mtakatifu daima dawamu yu pamoja na Yesu, hangojei kuondoka kwake ndio aje.
Alikuwa na Yohana Mbatizaji (Nabii Yahya) tangu tumboni mwa
mamaake. Luka hapo anatupa ushahidi kuwa Yohana hakupata kunywa divai
wala kileo "kwa sababu atakuwa mkuu mbele ya Mungu" . Ni nani,
basi aliyewahalalishia Wakristo kunywa ulevi, hata ikawa ibada yao haitimii ila
wanywe mvinyo? Labda ni Paulo akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ni kweli
wafuasi wa kweli wa Yesu sio wale wapigao kelele, Bwana, Bwana, sisi twaamini
uwokozi wa damu yako. Wafuasi wake wa kweli ni wale wanaotenda aliyofundisha,
na wanaokwenda mwendo wake. Hao hata hawana haja ya kujiita Wakristo.
Si kama Roho Mtakatifu alikuwa na Yesu tangu tumboni mwa mamaake tu kama
Yohana, bali tunaambiwa na Injili ya Mathayo kuwa hiyo mimba yenyewe kaichukua
mama yake, Mariamu, "kwa uweza wa Roho Mtakatifu." (Mathayo
1.18).
Ni wazi kabisa kuwa Roho Mtakatifu hakungojea Yesu aondoke ndio aje, bali daima
milele yupo, kwa ushahidi wa Biblia yenyewe. Kwa ushahidi huu tu tunayakinika
kuwa huyo Msaidizi ajaye, siye Roho Mtakatifu, nafsi ya pili ya Mungu.
Tena tunaambiwa kuwa Roho Mtakatifu ndiye anayeongoza Kanisa mpaka hii leo.
Lifanywalo na lisemwalo na Kanisa basi ni kwa uwongozi na ufunuo wa Roho
Mtakatifu, huyo aliyebashiriwa na Yesu kama ilivyosimuliwa katika Injili ya
Yohana. Lakini ilivyokuwa Ukristo ulivyogawika katika makanisa, au madhehebu,
yasiokuwa na hisabu, na kila kanisa linafunza mambo ambayo tangu msingi wake
yanakhitalifiana na mengineyo, jee ni madhehebu gani, au kanisa gani,
linaloongozwa na Roho Mtakatifu.
Kama wote hao wanaongozwa na Roho huyo huyo basi mbona wanagongana katika mambo
ya msingi? Bali hata kanisa moja, mathalan, Kanisa Katoliki la Roma, ndilo
kubwa lao na lenye nidhamu kuliko yote, mbona mara nyingi hugeuza geuza maoni
yake? Zamani tulipokuwa wadogo ilikuwa mwiko kwa Wakatoliki kula nyama
siku ya Ijumaa, kwa kuwa ndio siku aliyotundikwa Bwana Yesu. Sasa ni halali.
Zamani ilikuwa mwenye kuwa na wake zaidi ya mmoja akitengwa, na wala hapati
ibada fulani za sakramento, kama Kushiriki katika Chakula cha Bwana. Leo
wanakubaliwa, na inakubaliwa kuwa kuoa mke mmoja si sharia ya Kikristo bali ni
mila za Kizungu zilizoingizwa katika dini. Aliyewazindua Wazee wa Kanisa ni
Roho Mtakatifu? Ikiwa ni yeye kwa nini huyo Roho Mtakatifu alinyamaza
kimya miaka yote hiyo? Wangapi waliotengwa na Kanisa, wakalaaniwa, na wakachomwa
moto hadharani, na baadae watu hao hao baada ya miaka kupita wakaja wakatakaswa
na kubarikiwa na kutangazwa na Kanisa lile lile kuwa niWatakatifu? Na wakati
huo huo tuone ni Roho Mtakatifu, Mungu, asiyekosea, ndiye amelijaa Kanisa na
analiongoza! Bila ya shaka huyu siye aliyebashiriwa na Yesu. Kanisa la
Roma linasema ni haramu kwa padri kuoa. Hivi sasa wapo mapadri si chini ya
80,000 duniani wa Kanisa la Roma ambao wana wake, miongoni mwao 18,000 wako
Amerika (U.S.A.). Si ajabu kutokea siku yo yote kuwa Baba Mtakatifu, huku
akiongozwa na Roho Mtakatifu, akiona mambo ni ya mno, akatoa amri kuwa sasa ni
halali kwa mapadri kuoa bila ya kificho, na bila kuleta nuksani yo yote.
Yesu ametwambia kuwa huyo ajaye hatanena kwa shauri lake mwenyewe. Je, Roho
Mtakatifu, ambaye ni Mungu, hunena kwa shauri ya nani? Mungu hunena
anayoyasikia au hunena yake mwenyewe? Ikiwa hunena anayoyasikia, basi
anayasikia kwa nani? Kwa Mungu Baba, au kwa Mungu Mwana, na hali tunaambiwa
katika Utatu, nafsi zote tatu ni sawa. Ikiwa yeye ni Roho
Mtakatifu, ambaye ni Mungu, pana lipi la ajabu hata ihitajie Yesu kusema kuwa
atatoa habari ya mambo yajayo? Hapana ajabu Mungu kuagua yajayo, na hali ni
Yeye aliyeyaumba.
Huyo ajaye, Yesu anasema, atamtukuza Yesu. Kwani Mungu Mwana ana haja gani ya
kutukuzwa na Mungu Roho?
Hayo yote tukiyazingatia kwa nia safi tutaona kuwa hayamuelekei Roho Mtakatifu,
ambaye ni Mungu kama lisemavyo Kanisa, hata chembe. Je, kama bishara hii
haimuelekei Roho Mtakatifu, inamuelekea nani? Ni mtu gani huyo ambaye
alikuja ulimwenguni baada ya kuondoka Yesu, akauhakikisha ulimwengu kwa khabari
ya dhambi na hukumu, akauongoza ulimwengu na kuutia kwenye kweli yote, akawa
haneni kwa shauri lake wala mapenzi yake bali husema kwa aambiwayo na Mwenyezi
Mungu, akatoa khabari ya dhambi na mambo yajayo, akatwachia mafunzo katika
Kitabu kisichobadilika milele na mafunzo yake yakakaa nasi milele mpaka mwisho
wa dunia, akamtukuza Yesu Kristo? Katika historia yote hakutokea mtu
mwenye kukusanya sifa zote hizo ila Nabii Muhammad tu.
Mtume Muhammad s.a.w. ndiye aliyekuja baada ya Nabii Isa a.s. Yeye peke yake
katika Manabii na Mitume wote ndiye aliyesema maneno ya kutimiza ujumbe wote wa
Mwenyezi Mungu, ndiye aliyeleta kweli yote. Kila Nabii aliyetangulia
alibashiri kuja mwinginewe baadae. Musa alisema hayo, na Yesu kasema hayo, na
wenginewe wote wamesema. Ila Nabii Muhammad ndiye aliyesema: "Hapana
Nabii baada yangu." Na Mwenyezi Mungu alimwambia karibu ya kufa
kwake:
(Qur'ani) Al Maida 5.3
Mwenye
kukamilishiwa Dini na kutimiliziwa Neema, amekamilishiwa na kutimiliziwa kila
kitu: ndiyo kweli yote, na hukumu na khabari ya dhambi. Ni Muhammad ndiye
ambaye alikuwa akijuulikana hata na maadui wake kuwa ni msema kweli, wa
kuaminiwa, Assaadiq, Al Amin, "Mkweli Muaminifu" na kweli
ndiye Roho wa kweli.
Huyo ajaye, Yesu anatwambia, hatanena kwa shauri lake. Ni Mtume Muhammad,
peke yake, ndiye ambaye historia inatwambia kuwa mafunzo yake ni maneno ya
Mwenyezi Mungu. Qur'ani Tukufu yote ni maneno ya Mungu, moja kwa moja.
Qur'ani haikutungwa na Muhammad wala na ye yote katika wanaadamu. Sio
kama vitabu vya Biblia, ambavyo vinajuulikana vimeandikwa na watu fulani kama
vile Injili ya Mathayo, ya Marko n.k. na Torati ya Musa. Hii ni Qur'ani
ya Mwenyezi Mungu, si ya Muhammad. Kama isemavyo hiyo Qur'ani:
(Qur'ani) Arrahman 55.1-2
Na ilivyobainishwa katika Sura An Najm:
Wala (Muhammad) hasemi kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa; amemfundisha Mwenye nguvu kweli.
(Qur'ani) Annajm 53.3-5
Na
ilivyosemwa katika Sura An Nisaa:
(Qur'ani) An Nisaa 4.82
Mkristo
wa Kiingereza, Dr. John B. Taylor, Mwalimu wa Masomo ya Kiislamu katika Chuo
cha Birmingham, ameandika katika kitabu chake: Thinking About Islam
(Kuufikiria Uislamu):
Hayo ni maneno ya Mkristo ambaye kazi yake ni kuutafutia ila na nuksani
Uislamu. Qur'ani ni neno la Mwenyezi Mungu lisio na upungufu wo wote kwa
sababu ni maneno yake mwenyewe. Hayo ndiyo makusudio ya Yesu aliposema
kuwa huyo Msaidizi ajaye, "hatanena kwa shauri lake mwenyewe."
Yesu kadhaalika ametwambia kuwa Msaidizi atakayekuja atatoa khabari ya mambo
yajayo. Kila alilosema Mtume Muhammad s.a.w. kuwa litakuja basi limetokea vile
vile alivyosema. Katika alilosema ni kuwa Warumi baada ya kushindwa na Waajemi
wao watakuja shinda mnamo miaka michache na hapo Waislamu watafurahi. Na kweli
walishindwa Waajemi mwaka 624 B.K. na ndio mwaka Waislamu walipowashinda
makafiri wa Kikureshi katika vita vya Badru.
Mtume alipokubali mkataba wa suluhu pale alipozuiliwa kuingia Makka alisema
kuwa Waislamu watakuja kuikomboa Makka karibuni, na hakika hivyo ndivyo
ilivyokuwa baada ya miaka miwili, na ikawa ndio ushindi ulioenea Arabuni kote.
Mtume Muhammad alipokuwa akichimba handaki, pamoja na Masahaba zake, kuilinda
Madina na maadui, kulimetuka cheche tatu alipokuwa akipiga mtaimbo kulisukua
jiwe. Cheche moja ilielekea kusini, Mtume akasema Yaman itasilimu. Cheche ya
pili ikaelekea mashariki, na Mtume akasema Iran itasilimu. Cheche ya tatu
ilipometukia kaskazini Mtume s.a.w. akasema Sham iliyokuwa chini ya utawala wa
Kikristo wa Kirumi itasilimu. Na zote zikaja kusalimu amri na
kusilimu hivyo hivyo kama alivyobashiri, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, katika
zama ambazo Warumi walikuwa ndio kama Marekani walivyo sasa, na Waajemi ndio
kama Warusi walivyo sasa. Hizo ndizo dola kubwa kabisa, na Muhammad ni bedui
mnyonge ambaye ndiye kwanza kachipuka huko jangwani akiwahubiria makafiri wa
miji miwili midogo kabisa Makka na Madina. Na mengi, kabisa, aliyokuwa
akiyasema Mtume Muhammad s.a.w. na yote yalikuwa hayaanguki chini.
Nimeyataja hayo ambayo yamo katika vitabu vya historia vilivyoandikwa hata na
wasiokuwa Waislamu.
Yesu tena amesema huyo Msaidizi "atanitukuza mimi." Na kweli
Yesu Kristo au Isa Masihi (wamuitavyo Waislamu) alitukanwa na maadui
zake, Mayahudi, kwa kumwambia kuwa ati ni mwana haramu, mzushi, mlaanifu.
Wakidai kuwa uthibitisho wa laana hiyo ni kuwa waliweza kumwua kwa kumtundika
msalabani. Taurati ilisema kuwa ye yote anayekufa kwa kutundikwa kwenye mti basi
amelaanika, na hayo ndiyo yalikuwa makusudio yao. Hali kadhaalika waliokuwa
wakijiona kuwa ni wafuasi wake Yesu watiifu walimvunjia daraja yake kwa
kukubali madai ya Mayahudi kwa kuwa alikufa msalabani, na pia kwa kumfanya yeye
ni sawa na ile miungu ya bandia ya uwongo sawa na ya akina Mithra, na Apollo,
na Osiris ya kipagani, na kwa kumtoa kwenye cheo chake kitukufu ambacho yeye
mwenyewe alikuwa akitafakhari nacho kama isemavyo Biblia. Daima Yesu
akitafakhari na kujiita yeye ni mwanaadamu, mtumishi wa Mwenyezi Mungu, ambaye
hawezi kusema kitu wala kutenda kitu ila kama anavyoamrishwa na Mungu. Yesu
akitafakhari kuwa ni Nabii wa Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, sio kuwa mungu
kama miungu iliyojaa katika pande zile kwa zama zile. Hata wafalme madhaalimu
wa Kirumi walikuwa wakiitwa miungu. Wao hao wajiitao Wakristo waliacha
kufuata mafundisho yake Yesu na kuyatenda, na badala yake wakafuata mafundisho
ya wale wale washirikina ambao Yesu kaja kuwapinga. Ndio maana
akasema: "Wengi watanambia siku ile, Bwana, Bwana,
hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako
kufanya miujiza mingi? Ndipo nitwaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe
ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."
Ni kwa kupitia Mtume Muhammad, huyo Msaidizi aliyetwambia Yesu kuwa atakuja
kumtukuza, ndio tunasoma maneno ya Qur'ani Tukufu:
(Qur'ani) An Nisaa 4.171-172
Katika
Sura Al Imran tunasoma vipi alivyotukuzwa Yesu:
(Qur'ani) Al Imran 3.45-49
Na
kabla ya aya hizi inasimuliwa vipi alivyoteuliwa mama yake Yesu na kutukuzwa:
(Qur'ani) Al Imran 3.42