Makanisa
ya Kikristo yanafunza ya kuwa Yesu Kristo si kama kuwa ni Mwana wa Mungu tu,
bali hakika ni Mungu khasa. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni mmoja.
Watatu katika mmoja, na mmoja katika watatu. Wote ni wa milele, wote ni
sawa. Yesu ni Mungu, na Mungu ni Yesu. Hiyo ni imani ya Kikristo, ambayo
inaaminiwa na karibu Wakristo wote. Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema
nini katika jambo hili?
Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika:
1 Wakorintho 15.15
Juu ya
kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na
Mwenyezi Mungu ni kitu kimoja hapa anasema: "Tulimshuhudia Mungu ya
kuwa alimfufua Kristo." Ikiwa Mungu kamfufua Kristo, hawawezi kuwa
wote wawili hao ni mtu mmoja. Mmoja alikuwa ni mtenda, mfufuaji, na wa
pili alikuwa ni mtendwa, mfufuliwa. Kama Kristo ni Mungu mwenye uwezo wa
kufufua basi maelekeo ni kusema: "Kristo kajifufua", sio kafufuliwa.
Mwenye kufufuliwa ni mfu asiyejiweza kitu.
Katika kitabu cha Matendo ya Mitume inasimuliwa kuwa Mt Stefano alisema aliyoyaona
yaliyo mbinguni. Alisema:
Matendo
7.56
Mwana
wa Adamu ndiye Yesu, na kwa jina hilo ndio mwenyewe akipenda kujiita, sio Mwana
wa Mungu. Hapo basi huko mbinguni Stefano anasema anamwona Yesu kakaa mkono wa
kulia wa Mungu. Mwenye kukaa mkono wa kulia wa fulani hawezi kuwa ndiye yule
yule fulani. Hayo ni maelezo ya mbinguni. Ni wazi basi kwa ushahidi wa
Biblia kuwa Yesu hakuwa Mungu mbinguni kama alivyokuwa si Mungu duniani.
Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi
alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:
Luka 22.42-43
Hapa
tunaona mambo matatu muhimu:
Jee,
yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama
upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo
hadithiwa na Yohana kuwa kasema:
Yohana 14.28
Na
mwishoni naye yupo mslabani:
Mathayo 27.46
Yafaa
hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni
Mungu? Au nini alikusudia aliposema: "Mungu wangu naye ni Mungu wenu"?
Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu
mbele ya Mungu wake. La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na
kuvunjika moyo. Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa
Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Ama kuwa Mungu akate
tamaa na Mungu, na kumyayatikia: "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona
umeniacha", ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si
Yesu.