Tumekwisha ona kutokana na maneno ya Injili na maandiko mengine ya Agano Jipya tuliyoyanukulu kwamba Yesu ametumwa na Mwenyezi Mungu. Ametumwa awendee nani? Hebu tuiache Biblia itueleze:
Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawaMathayo 15.21-28
Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye
hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." Hakuwajia
Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina.
Mathayo 7.6
Mbwa na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa
Israili. Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi. Hayo ndiyo
mawazo ya Yesu, au ya hao walioandika Injili na wakatia maneno hayo kinywani
mwa Yesu.
Mathayo 9.12
"Upande mwengine, huku kutaja mbwa na nguruwe huweza kuwa ni maneno aliyoyachagua Mathayo kulipa nguvu wazo
Na juu ya kauli ya Yesu : "Si vema kukitwaa chakula cha watoto na
kuwatupia mbwa," Asimov anasema:
Tukiendelea na isemavyo Biblia juu ya ujumbe wa Yesu tunapata ushahidi zaidi
kutokana na Injili ya Mathayo:
Mathayo 10.5-6
Hao
Thenashara ni wanafunzi wake kumi na mbili aliowateua mwenyewe Yesu kutangaza mafunzo
yake. Hapo anawapa amri zilizo wazi kuwa wasiwaendee watu wa Mataifa,
yaani wasiokuwa Waisraili. Hao wanafunzi kumi na mbili ndio wanaoitwa katika
Biblia "mitume" kwa kuwa walitumwa na Yesu. Na wao kama yeye mwenyewe
hawakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa Israel" kwani "si vema
kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
Kwa nini Yesu alisema maneno kama haya ya kukataa na kukataza kuwafunza dini
ila Waisraili tu? Kwa nini alitumia mifano mibaya kama hivyo
"mbwa" na "nguruwe" kwa kuwakusudia hao watu wengine wasio
Mayahudi, yaani ndio mimi na wewe mwenzangu? Wataalamu wa Kikristo na
wasio Wakristo wamestaajabishwa na maneno hayo. Ni maneno machache katika
aliyoyasema Yesu ambayo yamewatatiza wasomaji Wakristo kuliko maneno haya.
Wapo wanaoona kuwa Yesu alitumia matusi yale kuwaita wote wasio Mayahudi
kufuata mwenendo wa Kiyahudi, yaani ndio hivyo Mayahudi wawaonavyo binaadamu
wote wasio kuwa wao. Na wapo wasemao kuwa Yesu akipenda kufunza kwa mifano, na
hivyo anafananisha kama kwamba yeye anaamini hiyo imani mbovu ya Kiyahudi ya
kudharau watu wasiokuwa kabila yao. Na wapo wengine kama Asimov ambao wanaona
maneno yale ni ya Mathayo, na yeye Mathayo (au ye yote yule aliyeandika Injili
hiyo) kamuambatisha nayo Yesu maneno hayo, kwa kuwa yeye mwandishi alikuwa
Mkristo wa kabila la Kiyahudi na anacho kiburi cha Kiyahudi.
Ama kusema kuwa hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa Israeli inaonekana kama
kilivyosema kitabu cha The Interpreter's Bible kuwa Yesu hakika kwanza aliamini
kuwa alitumwa kwa Waisraili tu. Ni jambo la kustaajabisha kuwa Mungu au
Mwana wa Mungu aje duniani atumwe na kwanza asiujue utumwa wake ila aamini tu
kuwa katumwa kwa watu wake wa Kiyahudi basi. Na kama yeye ni Mungu au
Mwana wa Mungu, katumwa na nani? Kama katumwa na Mungu, basi yeye si
Mungu. Si hilo tu, bali hata akiwa ni Nabii na Mtume wa Mungu tunamtaraji
aujue tangu mwanzo huo ujumbe wake aliokuja nao, asiwe kutapatapa,
kupapasa, na kuhangaika katika jambo la msingi.
Hapana haja ya kuyatafutia tafsiri hii na maana hii, hayo maneno yaliyo wazi ya
Yesu Kristo. Yesu hakika hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya
Israeli. Yesu hakika kawakataza "mitume" wake wasende
kuwahubiria mataifa mengine. Yesu ni kweli kaonya kuwa kuwafundisha
mafunzo yake hayo mataifa mengine ni sawa sawa na kuwapa mbwa kilicho
kitakatifu, na kuwatupia lulu nguruwe. Kwa nini ikawa hivi? Ikiwa Yesu kweli
katumwa na Mungu, kwa nini ujumbe wake uwekewe mipaka kwa jamaa zake tu wa
Kiisraili, na yeye asikiuke mipaka ile? Naam, zipo sababu zenye nguvu kwa
hayo.
Kwa hakika hayo hayakuwa mageni, wala Yesu hakuwa Mtume wa mwanzo kutumwa hivyo
na Mwenyezi Mungu. Mitume wote waliokwisha kuja kabla yake walikuwa ni
Mitume wa vikundi vyao tu, na zama zao tu, na walikuja na mafunzo yao maalumu machache.
Musa alikuwa hivyo, na Yesu hali kadhaalika. Hali yake hali ya wenziwe,
ila yeye alikuwa ndiye Mtume wa mwisho katika Mitume waliotumwa kwa kabila
maalumu. Kwa nini Mwenyezi Mungu akafanya hivyo?
Kwa nini Yesu alikatazwa, mathalan, asiwahubirie yeye wala wafwasi wake,
Waafrika, au Wazungu, au Wahindi, au Machina, au Waarabu? Amekatazwa kwa
sababu kabila zote hizo zilikuwa hata hazijachukua khatua ya mwanzo ya kuamini
Mungu Mmoja. Kabila hizo na mataifa hayo yalikuwa makafiri ama wa kuabudu
masanamu, au kuabudu mapango au miti au viumbe vyengine au kuabudu wanaadamu
wenzao. Na ujumbe wake Yesu ni kutengeneza mwenendo, tabia ya watu ambao
tangu hapo wanayo imani ya Mungu mmoja. Yeye hakuwa na uwezo wala muda wa
kujenga tangu chini. Yeye kazaliwa katika umma wenye kuamini Mungu Mmoja,
umma wenye sharia ya Mwenyezi Mungu. Kazi yake kwa muda mchache alioishi
na kuhubiri ni kiasi ya kuwapiga msasa tu Mayahudi ambao walikwisha tahiriwa,
wanajua cha halali na haramu, na muhimu kabisa wanamjua Mwenyezi Mungu Mmoja,
asiyezaa wala kuzaliwa. Ila yao Mayahudi ni kutokuwa na huruma, na
kuifanya dini sharia tu isiyo na roho na imani. Mayahudi waliishika sharia ya
Musa kwa dhaahiri yake, lakini waliutupilia mbali uchamngu wa Ibrahimu,
wakashika ya kuonekana na watu, na wakatupa ya ndani anayoyaona Mwenyezi Mungu
na dhamiri zao. Walipoacha "mitume" wa Yesu amri hiyo ya Mungu
ya kutowendea makafiri wasiomjua Mungu wala msingi wa sharia, ndipo mafunzo ya
Yesu yalipochafuka. Kwani hao makafiri walipoingia katika Ukristo
walijigeuza jina tu, lakini waliingiza karibu yao yote ya kikafiri katika dini
ya Yesu, ikaitwa Ukristo, na hali sio Ukristo kabisa aliyoufundisha Yesu.
Mahekalu yao ya kipagani yakageuzwa makanisa, na mizimu na mapango yao yakawa
ndio monastari za Kikristo. Lau kuwa Wana wa Israili wangeli mwitikia Yesu,
basi Ukristo usingelichafuka kama ulivyo chafuka.
Upton Sinclair akiandika juu ya wakati ilipoingia Dola ya Kirumi katika Ukristo
na ikaufanya ndio dini rasmi ya taifa, amesema kwa masikitiko: "Ulikuwa ni
ushindi kwa Kanisa, na kwa mwenyewe mwenye kuanzisha (yaani Yesu) ni kushindwa
kwa muda. Maana yake ni kuwa maadui zake wamelichukua jina lake, mafunzo yake,
na nguvu zake."
Yesu alionya, lakini Paulo hakusikia:
Yaliyosemwa yamekuwa. Kwa kitendo cha Paulo kuwaingiza mapagani wa
Kizungu katika dini ya Yesu sharia ya Mwenyezi Mungu ikaambiwa ni laana,
ikatolewa ruhusa kula nyamafu, nguruwe na damu, na kila kiuzwacho sokoni bila
ya kutia wasiwasi wo wote katika dhamiri. Tohara aliyoamrishwa Ibrahimu na
Mwenyezi Mungu na Manabii wote wakaifuata mpaka mwenyewe Yesu na wanafunzi
wake, Paulo aliipuuza kuwaridhi makafiri. Imani za kipagani za mungu mwana na
utatu zilizoenea katika mila za Mithra, Osiris, Attis n.k. zikaingizwa katika
dini ya Kikristo.
Katika ufalme wa mbinguni Yesu ana yakini kuwa hatokuwa nao ila wana wa Israili
tu. Injili ya Mathayo inasema:
Mathayo 19.28
Hata katika
maombi yake inaonyesha kuwa Yesu alikuwa anajua mipaka yake na uwezo wake.
Madai ya kuwa yeye ni mwombezi, mbali kuwa ni mwokozi, wa ulimwengu mzima ni
kumsingizia jambo ambalo mwenyewe hakulidhania. Kumpa mtu cheo asichokuwa nacho
ni kumtukana, ni kumvika kilemba cha ukoka, kama Mayahudi walivyotaka kumkejeli
kwa kumvika taji la miba. Cheo alicho nacho kwa hakika si kidogo. Kuwa ni
Mtume wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Mitume na Manabii watukufu ni jambo kuu
kweli kweli. Kuwa mtumishi wa Mwenyezi Mungu mwenye kupendeza si utukufu mdogo.
Na Yesu alitafakhari nao, na alitafakhari kuwa yeye hakutumwa ila kwa
kondoo waliopotea wa Ki-Israili. Na hayo si kwa upungufu wo wote kwa upande
wake, ila ni kuutumikia ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa kuulinda usiharibiwe na
washirikina mpaka ufike wakati wa kuja huyo atayekuwa kazi yake ni kuitangazia
risala ya Mungu kwa ulimwengu mzima.
Katika Injili ya Yohana ananukuliwa Yesu kusema:
Yohana 17.9
Tukiyachungua
vilivyo maneno ya Yesu kama yalivyosimuliwa na Mathayo na Marko ya kuwa yeye
alitumwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israili, na maamrisho yake yalio
wazi kuwapa "mitume" wake wasende kwenye mataifa mengine isipokuwa
Mayahudi tu, na kuwa yeye na wanafunzi wake kumi na mbili watakaa katika viti
vyao vya utukufu wakizihukumu kabila kumi na mbili za Israili katika ulimwengu
mpya wa mbinguni, hatuwezi ila kuhukumu kuwa hao watu anaowaombea Yesu ni hao
hao waliokwisha tajwa kabla, yaani wana wa Israili, sio ulimwengu, sio mimi na
wewe. Mimi na wewe si Wana wa Israili. Mimi na wewe ni mataifa
mengine. Mimi na wewe na ulimwengu, usiokuwa wa Kiyahudi, Yesu kesha sema
hatuombei, ikiwa tutakubali maneno yaliyoandikwa katika Injili zote.
Ni jambo linalojuulikana katika historia - na hata ukisoma katika Biblia kitabu
cha Matendo ya Mitume utaona - ya kuwa Ukristo kwanza haukuhubiriwa kwa mataifa
mengine mpaka alipoingia Paulo. Na yeye alipingwa vikali sana kwa kutoa shauri
hiyo na wanafunzi wake Yesu waliomwona na wakawa naye siku zote na wakajifunza
vilivyo mafunzo yake na makatazo yake ya kwenda kuwahubiria watu ambao bado ni
makafiri. Dr. Marcello Craveri anaandika katika kitabu chake The Life
of Jesus:
Mtaalamu wa Biblia, Dr. Hugh Schonfield, katika kitabu chake, Those
Incredible Christians, (Wale Wakristo wa Ajabu) ameandika juu ya Paulo na
ugomvi wake na wafuasi wa kweli wa asli wa Yesu hivi:
Busara ya Mwenyezi Mungu kukataza mafunzo ya Yesu yasikiuke mipaka ya Israili
ni kuwa isije dini ya haki ikaharibiwa na ushirikina wa makafiri ulioenea pande
zote katika zama zile. Ulimwengu ulikuwa bado haujawa tayari kupokea ujumbe wa
ulimwengu mzima, na huyo mwenye kuweza kubeba ujumbe ule hajazaliwa, na umma wa
kutimiza jambo hilo na kulieneza bado haujapikika ukawa tayari. Yaliyotokea
tumeyaona. Ukristo tuuonao na ulioenea ulimwenguni sio Ukristo aliofundisha
Yesu. Wa Yesu ulitoweka na mwenyewe na wafuasi wake wa mwanzo wa kabila la
Kiyahudi. Paulo kaufuja Ukristo.
Kauli zinazonukuliwa kwa kudai kuwa ni ushahidi kuwa Yesu mwenyewe alitaka
mafunzo yake yakafundishwe kwa ulimwengu wote yamo katika Injili ya Mathayo
28.19-20, Injili ya Luka 24.46-49 na Marko 16.15.
Mathayo inasema:
Mathayo 28.19-20
Luka
anatwambia:
Luka 24.46-49
Na
Injili ya Marko inasema:
Marko 16.15
Je,
imekuwaje? Yesu ni kigeugeu? Mbona huku anawakataza wanafunzi wake
wasende kuwahubiria ila kabila kumi na mbili za Israili, na huku anawaambia
nendeni kuwahubiria Injili ulimwengu mzima. La, Yesu si mbabaishi, wala
si kigeugeu. Hebu natuziangalie vilivyo hizo amri mbili, moja ya kuwa mafunzo
yake wasifunzwe ila wana wa Israili tu, na ya pili ni hii ya kuwa watu wote
wafunzwe dini.
Vipande vyote vitatu tulivyonukulu mwishoni havitaji mambo ya Yesu alipokuwa na
maisha yake ya uhai wa kidunia, lakini vyaeleza mambo yaliyotukia baada ya
"kufufuka kutoka wafu" kama inavyosimuliwa na Injili zote tatu.
Yajuulikana kuwa Injili ya mwanzo kuandikwa ni Injili ya Marko. Hizo
nyingine ziliandikwa baadae, na labda ujuzi wao ulitegemea hiyo hiyo Injili ya
Marko. Yajuulikana vile vile kuwa maneno yote yaliyohusu kufufuka Yesu kutokana
na wafu, pamoja na hayo maamrisho ya kwenda kuihubiri Injili "kwa kila
kiumbe", kinyume na maamrisho yake yote ya kuwa asihubiriwe ila Muisraeli
tu - maneno hayo yote hayakuwamo katik Marko ya asli, bali yaliongezwa baadae.
Encyclopaedia Brittanica, nakla ya 11, jalada 17, sahifa 730, yasema ya
kuwa kipande chote hicho kiliongezwa baadae, yamkini mwanzo mwanzo wa karne ya
pili, kuchukua maneno yaliyopotea, au yaliyoonekana kuwa ni mapungufu.
William Neil akiandika katika tafsiri ya Biblia iitwayo Harper's Bible
Commentary anasema:
Maneno hayo ya Paulo aliyowaandikia Wakorintho na ndio mara ya kwanza kutajwa
kufufuka kwa Yesu ni haya:
1 Wakorintho 15.3-8
Ikiwa
kipande chote tangu mstari 9 mpaka mstari 20 katika sura 16 ya Injili ya Marko,
kimepachikwa, basi kisa chote cha kufufuka Yesu kimebuniwa. Mwenye kubuni
kisa hichi ni Mtakatifu Paulo. Hivyo ndivyo tunavyoweza kuagua kutokana
na kuisoma Biblia, kwani maandishi ya kwanza hayamo katika Injili bali yamo
katika barua ya Paulo kwa Wakorintho.
Amesema Craveri katika Maisha ya Yesu:
Ikiwa basi msingi wa hadithi nzima ya kufufuka Yesu hadi ya ubora wake ni kuwa
ni ya shaka shaka - licha ya kuwa ni wazi kuwa ni ya uwongo - hapana njia ya
kuamini ya Kuwa Yesu wakati wo wote katika historia aliwahi kuamrisha watu
"Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina
la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu," kwa sababu haya hakuyasema ila
baada ya huko kunakoambiwa ni kufufuka.
Katika Biblia ya Kiswahili iliyo mbele yangu iliyotangazwa na The British
and Foreign Bible Society 1950 kifungu cha Marko 16 tangu mstari wa 9 mpaka
mwisho yaani mstari wa 20 kimetiwa katika mipinde miwili hivi ( ) kuonyesha
kuwa maneno hayo hayakuwamo katika maandiko ya asli. Ilivyokuwa imethibitika
kuwa hayo ya Marko si madhubuti, basi yaliyonukuliwa na Mathayo na Luka juu ya
mambo hayo ya kufufuka, na kuamrisha kwenda kuhubiria watu wa ulimwengu, na
kuutaja Utatu, yote hayo ni baatili.
Kwa mukhtasari tunaona kuwa Biblia inashuhudia kuwa Yesu alikuwa ni Nabii
aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa Waisraili waliopotea njia. Hadithi ya
kuwa aliamrisha mafunzo yake yakatangazwe kwa watu wote "kwa jina la Baba,
na Mwana na Roho Mtakatifu" imebuniwa na kuongezwa mwishoni mwa Injili
tatu za Mathayo, Marko na Luka. Kadhaalika kuwa Yesu alifufuka kutoka
wafu kwa njia ya kimiujiza imeongezwa, na kauli ya Utatu basi ya kuwa mafunzo
yakatangazwe "kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu" pia nayo
imebuniwa na wala haina asli yo yote ya kweli.