Katika
Injili nne ziliomo katika Biblia Yesu Kristo ametajwa mara kadhaa wa kadhaa kwa
jina la "Mwana wa Mungu". Ifuatayo ni baadhi ya mifano yake:
Marko 15.39
Huyo
akida anayetajwa hapo juu ni mpagani wa Kirumi mwenye kuamini wanaadamu
wanakuwa miungu, hata mfalme wao wakimwita kuwa ni mungu na mwana wa mungu.
Luka 1.35
Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.
Luka 22.70
Mathayo 27.43
Marko 3.11-12
Mathayo 8.28-29
Katika
Injili za Mathayo, Marko na Luka, Yesu ameitwa mara 22 kwa jina la "Mwana
wa Mungu", lakini hata mara moja yeye mwenyewe hakujiita kwa jina
hilo. Katika Mathayo 27.43 tuliyonukulu hapo juu yanatajwa maneno ya
wakuu wa makuhani wa Kiyahudi pamoja na waandishi na wazee waliokuwa
wakimdhihaki, si maneno yake yeye Yesu. Hao walikuwa wakimzulia kuwa anadai
uwana wa Mungu, na anadai kuwa ni Mfalme wa Israeli. Aghlabu waliokuwa
wakimwita Mwana wa Mungu walikuwa ama wendawazimu, wenye pepo wachafu, au
askari wa Kirumi ambao tokea hapo wao ni washirikina, mapagani. Ama mwenyewe
Yesu alikuwa daima akipendelea kujiita mwana wa Adamu kwa Kiebrani, lugha yake,
Bin Adam, yaani ni binaadamu, mtu tu. Katika Injili jina hili la Yesu kuitwa
mwana wa Adamu limetajwa yapata mara 80. Makhasimu zake wa Kiyahudi
walimzulia kuwa alidai kuwa ni Mfalme wa Mayahudi ili kumchongea kwa watawala
wa Kirumi, na kuwa alidai kuwa ni Mwana wa Mungu ili apate kuchusha kwa
Mayahudi.
Francis Young, Mwalimu wa mafunzo ya Agano Jipya katika Chuo Kikuu cha
Birmingham, Uingereza, akiandika katika kitabu kinachoitwa The Myth of God
Incarnate (Uwongo wa Mungu kuwa Mtu) anasema:
Majina haya, basi, ya "mungu", "mwana wa mungu" na
"Bwana" kwa kuwa yalikuwa yameenea na maarufu katika nchi za bahari
ya Kati (Mediterranean) katika zama za Yesu haiwezi kukosa kuathiri
mawazo ya watu ambao bado haijawavaa imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja kama
ilivyokuwa ikifunza dini ya Kiyahudi. Majina kama hayo yalikuwa
yakitumiliwa ovyo na kila mtu takriban.
Na hizo hadithi za watu kama hao, ikiwa ni watu wa hadithini tu si wa kweli
kweli, au watu walioishi kweli kweli duniani, zimefanana mno na hizo ambazo
khalafu yake zikaaminiwa na Wakristo kuwa zimemkhusu Yesu Kristo peke yake.
Francis Young katika insha yake inayoitwa Mizizi Miwili au Matatanisho (Two
roots or a Tangled Mass) ameandika:
Tukirejea kuyanukulu yaliyomo katika Biblia tunamwona Yesu
mahkamani alikataa kukiri mashtaka aliyoshtakiwa kuwa yeye alidai kuwa ni Mwana
wa Mungu,
Mathayo 26.62-64
Injili
tatu za Mathayo, Marko na Luka (ambazo zimefanana) hazimtaji kabisa Yesu kuwa
ni Mwana "Pekee" wa Mungu. Ni Injili ya Yohana tu ndiyo
iliyokazania kumpa ungu Yesu na kumwita Mwana Pekee wa Mungu. Injili ya
Yohana inasema:
Yohana 1.14
Lugha
ya Yohana ni ya namna ya peke yake. Injili tatu za mwanzo, Mathayo, Marko
na Luka zinamweleza Yesu ni binaadamu. Lakini Yohana amepindukia mipaka hapa
kwa kumweleza Yesu kuwa ni "Neno" kwa maana aliyoipata kutokana na
waandishi wa Kigiriki, sio kutokana na maandishi ya Kiyahudi. Kauli hii
haikutajwa katika Injili hizo tatu za mwanzo wala katika vitabu vyote vya Agano
la Kale. Katika karne ya sita kabla ya Yesu kulizuka katika maifalasufi wa
Kigiriki nadhariya ya kuwa uumbaji wa ulimwengu haukuzuka ovyo lakini kwa
mpango wa kiakili, na ulimwengu wote unaendeshwa kwa kufuata sharia maalumu.
Sharia hii au akili hii au mpango huu waliuwita "Logos", maana
yake ni "Neno". Tunaona tamko hilo linatumika katika "Bio-logy"
"Geo-logy" "Psycho-logy", kwa maana ya "ilimu".
Katika zile zile zama za Yesu alikuwako mwanachuoni wa Kiyahudi katika mji wa
Iskandaria katika Misri ambaye alikuwa ni mwanachuoni katika ilimu za Kiyahudi
na vile vile ni mtaalamu katika falsafa za Kigiriki. Alijaribu kutaka
kueleza mafunzo ya Kiyahudi kwa kutumia hoja za falsafa za Kigiriki. Yeye
alitumia hii kauli ya Logos au "Neno" kwa kueleza ile hekima na
busara ya Mwenyezi Mungu katika kuumba. Myahudi huyu akiitwa Filo. Yohana
aliitumia lugha ya huyo Filo na kuingiza ndani yake mawazo ya kipagani
akachanganya falsafa ya Kigiriki kwa kumuambatishia Yesu, na kumfanya yeye Yesu
ndiye "Logos" au "Neno" na hilo "Neno" lilikuwapo
tangu mwanzo, na hilo "Neno"lilikuwa pamoja na Mungu, bali ndilo
khasa likawa ni Mungu. Haya yote hayakusemwa kabisa na Injili zote
zilizotangulia, wala Yesu mwenyewe hakuyadai, wala wanafunzi wake hawakupata
kumdaia. Tena Yohana alizidi kusema:
Yohana 3.16
Tunaona
kwa mara ya kwanza Yesu kuitwa Mwana wa Mungu wa pekee. Lakini hata kulitumia
neno "Mwana wa Mungu" kuna maana gani khasa? Tukiipitia Biblia
na kufungua sahifa zake tutaona kuwa jina hilo limetumiliwa kwa watu wengi
licha Yesu. Katika Agano la Kale ambalo lote limeandikwa hata kabla ya
Yesu hajazaliwa tunakuta mifano kama hii:
Mwanzo 6.1-2
Ayubu 38.6-7
Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari, usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai.Hosea 1.10
Ni dhaahiri tunaona ilikuwa ni jambo la kawaida hata kwa
waandishi wa Kiyahudi wanaoamini Mwenyezi Mungu mmoja kutumia maneno
Mwanachuoni wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri, aliyeandika kitabu chake,
Maisha ya Yesu (The Life of Jesus), anaamini kuwa neno
Lugha ya Kiyahudi ya Kiebrani na lugha ya Kiarabu zina asli moja. Mfano wa hayo
ni kama mathalan kutumia neno la Kiarabu Abd kama katika "Abdu-Llahi"
kwa maana ya "Mtumwa wa Mwenyezi Mungu",na likaja baadae kugeuzwa na
kubuniwa neno
"Ghulam" ambalo lina maana ya "Mtumishi" na vile
vile "Kijana". Na khatimaye likatumiwa neno "Ibn"
ambalo maana yake ni "Mwana" tu.
Hii ndio shida inayompata mtu ye yote anapotaka kujua hakika ya mafunzo ya
Kikristo. Hapana kitabu cho chote duniani chenye asli ya matamshi yake
Yesu wala wanafunzi wake. Wao wakisema Kiaramia, lugha ya mazungumzo zama zile
huko Palastini, kama ilivyo lugha ya Kiswahili kwetu. Na lugha yao ya
dini ni Kiebrania, kama ilivyo lugha ya Kiarabu kwa Waislamu po pote pale
walipo, au Kilatini kwa Wakatoliki. Injili zote ziliopo hapana hata moja
iliyoandikwa na kubaki katika lugha ya Kiebrania ya asli, ambayo tungeweza
kuirejea tupate ukweli wa kauli za Yesu. Ziliopo zote ni tafsiri za
Kigiriki. Injili za Kiebrania ziliamrishwa zote zichomwe moto. Hiyo
ni amri ya Wazee wa Kanisa, na ye yote aliyeonakana nayo hukumu yake ilikuwa
kifo. Inakubaliwa pia kuwa Injili zote zimeandikwa miaka mingi baada ya Yesu kwisha
ondoka duniani, na zimeandikwa na watu ambao hawakumwona bali ni kwa kufuata
masimulizi waliyoyasikia. Na ziliopo ni tafsiri, na tafsiri za tafsiri.
Yesu hakusema maneno yake kwa Kiswahili, wala Kiingereza, wala Kilatini wala
Kigiriki. Kama si kwa Kiebrania basi akifunza kwa lugha iliyofanana nayo, nayo
ni Kiaramia.
Hata bila ya ubabaishi wa tafsiri ni jambo la hakika kuwa katika maandishi ya
vitabu vya Biblia hili neno "mungu" likitumiwa ovyo. Tunasoma katika
Agano la Kale Mwenyezi Mungu anamwambia Musa vipi yatavyokuwa makhusiano yake
na nduguye Haruni:
Kutoka 4.16
Angalia
tena isemavyo Zaburi:
Zaburi 82.6
Utumiaji
ovyo ovyo maneno hayo matakatifu kama "Mungu" au ya kufuru kama
"mwana wa Mungu" yaliyotumiwa na waandishi wa Biblia yaonyesha wazi
vipi imani na agano la Ibrahimu na Manabii wengine walilofungamana kwalo na Mwenyezi
Mungu lilivyopotoshwa. Mayahudi ambao kumshirikisha Mwenyezi Mungu na cho chote
ni mwiko walishawishiwa na watawala wao na makafiri waliokuwa wakikaa nao
kutumia lugha na maneno ya kikafiri bila ya wenyewe kutambua. Sisi tunaona vipi
hii leo tulivyoharibiwa hata Kiswahili chetu na watawala ambao mila na dini zao
ni mbali na yetu. Tunaona vipi maneno kama "Halali na Haramu"
yalivyopotoshwa hata imekuwa yanatumiwa kuwa ni kilichoruhusiwa au kukatazwa na
serikali au chama kinachotawala, wala sio kama ilivyo asli kuwa alichohalalisha
na kuharimisha Mwenyezi Mungu. Tunasikia inasemwa kuna pombe ya
"halali", yaani inayoruhusiwa na serikali. Tunasikia kuna majumba au
mashamba yaliyopokonywa (kughusubiwa) na serikali yanaambiwa ati
"yametaifishwa" kihalali. Na ilhali hapana unyan'ganyi, au wizi wa
halali. Yote ni haramu. Hata hili neno "sharia" limepotoshwa
pia. Sharia ni sharia ya Kiislamu tu. Ya Serikali ni "Kanuni" si
sharia. Sharia ni ya Mwenyezi Mungu. Makosa anayoyafanya mcheza mpira (faul)
sasa yanaitwa: Dhambi. Badala ya Nguzo Tano za Uislamu watoto wetu wanafunzwa
"Nguzo tano za ujamaa".
Ni namna hivyo basi waandishi wa Biblia wa Kiyahudi ambao walikuwa wakimuamini
Mwenyezi Mungu mmoja waliikoroga lugha yao kwa kuwa maneno ya kikafiri ya
watawala wao wa kipagani wa Kirumi na jirani zao mapagani wa Kigiriki, wa
Kimisri na wengineo waliokuwa katika pande zile za mashariki ya Bahari ya Kati
(Mediterranean Sea) yaliwaathiri hata wao wakawa wanayatumia kama jambo
la dasturi.
Tuliyokwisha kuyanukulu ni maneno ya kutokana na sehemu ya Biblia iitwayo Agano
la Kale, yaani ile sehemu iliyoandikwa kueleza mambo ya Manabii waliokuwa
kabla ya Yesu. Hebu tuangalie sasa yaliyosemwa na Agano Jipya lilioandikwa
baada ya Yesu. Luka anatusimulia katika Injili yake alivyohubiri Yesu:
Luka 6.35
Hapo
twaona Yesu anawaambia wafwasi wake kuwa katika malipo ya watendao mema na
kuwapenda maadui zao ni kuwa watakuwa "wana wa Aliye juu" yaani
Mwenyezi Mungu. Katika Injili ya Mathayo Yesu anasema:
Heri wapatanishi;
Mathayo 5.9
Ni wazi
kwa maneno haya kuwa Yesu hakujiona yeye kuwa ni "mwana wa Mungu" kwa
maana ya namna ya peke yake kama linavyofundisha Kanisa. Kwa mujibu wa Biblia
wote watendao mema, wapatanishi, wanaokopesha bila ya kutaraji kulipwa n.k. ni
"wana wa Mungu". Hiyo ndiyo lugha ya Kibiblia, ndiyo lugha
iliyokuwa ikitumiwa wakati huo. Nasi tutakuwa wajinga tukimsikia mtangazaji wa
redio au T.V. kwenye uwanja wa futboli akisema: "Kafanya dhambi" kwa
kuwa mchezaji kaugusa mpira kwa mkono, nasi tukaamini kuwa yule mtu kweli
kafanya dhambi tunayoijua sisi, yaani kamkosa Mwenyezi Mungu na hivyo
anastahiki kutiwa katika jahannam! Haya yanadhihirika wazi katika hadithi hii
inayosimuliwa katika Injili ya Yohana. Mayahudi walipotaka kumpiga mawe Yesu
aliwauliza kwa vitendo gani vyema alivyowaonyesha ndio wanampiga?
Yohana 10.33-36
Kwa
mujibu wa kauli hiyo iliyoelezwa na Yohana tunafahamu kuwa Yesu anawaambia
Mayahudi kuwa ikiwa katika vitabu vyao watu wema wote wameitwa "wana wa
Mungu" pana ajabu gani basi kuwa Mtume wa Mungu aliyetakasika akaitwa vile
vile ni "mwana wa Mungu" kwa maana hiyo ya jumla jamala. Na
haya yanawekwa wazi na maneno aliyoyanukulu huyo huyo Yohana kuwa Yesu
akimwambia Mariamu Magdalene:
Yohana 20.17
Hata
Paulo naye amesema katika barua yake aliyowapelekea Warumi:
Warumi 8.14
Yohana
na Paulo ndio wakubwa wa kumfanya Yesu ni Mungu, au mwana wa Mungu, lakini hata
wao wametoa ushahidi wa kutosha kuwa huo "uwanamngu" wa Yesu ndio ule
ule kama walio nao wote walio wema.
Mwandishi wa Kimarekani maarufu, Upton Sinclair, akiandika katika kitabu chake A
Personal Jesus (Yesu Mtu) amesema: