Hebu sasa natulichungue hili neno lililofasiriwa Msaidizi
katika Bibilia ya Kiswahili, na ambalo limeitwa "Comforter"
yaani Mliwazi katika Biblia ya Kiingereza ya zamani ya King James, na
likaitwa "Counsellor", yaani Mshauri katika Biblia ya
Kiingereza ya Revised Standard Version, na likaitwa "Helper"
yaani Msaidizi katika Biblia za Kiingereza mpya mpya kama New World
Translation na Good News Bible, na "Mu'azzi", yaani
Mliwazi katika Biblia ya Kiarabu ya Darul Kitabul Muqaddas ya
Cairo.
Taabu inayotupata katika
kuisoma Biblia ni kuwa asli ya maandiko yote yamepotea. Tumebakiwa na nakala za
tafsiri tu. Na hata tukipata kwa mfano Injili ya Yohana iliyoandikwa kwa
lugha ilioandikwa mwanzo, nayo ni Kigiriki, hatuna ushahidi wo wote kuwa ndivyo
ilivyoandikwa hapo mwanzo. Injili hii iliandikwa mwanzo wake kiasi miaka
mia baada ya Yesu. Lakini nakala zilio kongwe kabisa zinazopatikana si
chini kuliko miaka mia mbili baada ya kuandikwa kwake.
Hali kadhaalika maneno aliyoyasema Yesu tunayapata kwa tafsiri tu, kwani Yesu
hakusema Kigiriki wala Kilatini, bali lugha ya kawaida Palastina wakati ule
ilikuwa ni Kiaramiya na lugha yao ya dini ni Kiebrania. Zote mbili hizo
zina asli moja na Kiarabu. Injili ya Yohana ndio hiyo iliyotaja hiyo bishara ya
Yesu kuwa atakuja huyo aitwae Msaidizi. Katika utangulizi wa nakla ya
Biblia ya Revised Standard Version imeelezwa kuwa hata hiyo matini ya Kigiriki
ilioko "imeharibiwa na makosa yaliyojumlika kwa kukosoea kosea kwa walionukulu
muda wa karne kumi na nne." Wataalamu wa Biblia wakubwa kama Rudolf
Bultmann (Mprotestanti) na Father John Lawrence Mackenzie (Mkatoliki)
wanakubali kuwa sehemu nyengine za Injili si kweli kihistoria, na ya kwamba
maneno fulani ya Yesu kwa hakika yamebuniwa na Kanisa la kale. Ye yote
asomae maandishi ya wataalamu wa Kikristo wenyewe, bali hata mwenye kusoma hizi
hizi tafsiri za Biblia mbili tatu ataona vipi maneno yanavyogeuzwa,
yanavyoongezwa, na yanavyopunguzwa, hata kugeuza kabisa makusudio. Encyclopaedia
Brittanica (nuskha ya 15) baada ya kueleza hayo imesema: "Ushahidi
kuwa hayo hakika yametokea ni mwingi na wa namna mbali mbali." Qur'ani
inasema:
(Qur'ani) Al Imran 3.78
Je, ni neno
gani hilo lilioandikwa Kigiriki kuwa Yesu kalitumia hata wengine wakalifasiri
Mliwazi, wengine Mshauri, na wengine Msaidizi, kuwa ndiye wa
kutarajiwa kuja? Nakla kongwe kabisa iliyopo ya hiyo Injili imetumia neno
la Kigiriki Parakletos ndilo wanalolifasiri Msaidizi katika Injili ya
Kiswahili. Katika Kamusi la Kigiriki neno Parakletos linafasiriwa kuwa
ni "mwenye kuitwa kusaidia, mtetezi, mwombezi." Baada ya
kuzingatia hayo tuliyoyasema hapo juu vipi yalivyogeuzwa geuzwa maneno, basi si
jambo la kustaajabisha ikiwa neno hili Parakletos nalo wamelipotoa waandishi na
wanaonukulu kwa karne na karne zilizopita, kama ilivyosemwa katika utangulizi
wa Biblia ya Kiingereza ya Standard Revised Version. Tunajua vipi
Wazungu walivyolipotosha jina la Muhammad, na kuliandika
"Mahomet". Hali kadhaalika neno la Kigiriki la Periklitos
ni wepesi kulipotoa na kuliandika Parakletos. Kwa dhaahiri
khitilafu ni ndogo, lakini kwa hakika neno Periklitos maana yake ni Msifiwa,
ambalo kwa Kiarabu ndio khasa Muhammad au Ahmad au Mahmuud. Jambo la
ajabu ni kuwa tangu wakati wa Yesu hapakutokea Mwaarabu mwenye jina hilo ila
huyo Muhammad bin Abdullah, ambaye alipewa jina hilo na babu yake tangu
kuzaliwa kwake bila ya kujua huyo mzee kuwa mjukuu wake atakuja kuwa Nabii
ambaye amebashiriwa na Yesu. Na huyo babu hakuwa Mkristo bali alikuwa
akifuata mila ya kishirikina na wala hakuijua Taurati wala Injili. Na
wala hakutokea Giriki mwenye jina la Periklitos.
Ni makosa kusema kuwa huyo Periklitos (Msifiwa) aliyefasiriwa kwa
kukosea Msaidizi, ni Roho Mtakatifu, ambaye Wakristo wanasema ni nafsi ya
Mungu. Ushahidi wa makosa hayo umo humo humo katika Injili ya
Yohana. Kama huyo Msaidizi ni Roho Mtakatifu yawaje basi Yesu kusema "yawafaa
ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo (Periklitos)
hatakuja kwenu." Roho Mtakatifu twaambiwa ni Mungu wa milele. Je,
kwani Mungu hatokuwepo maadamu Yesu yupo? Je, yeye Yesu na Manabii wote
waliomtangulia na watakatifu wengine hawakuteremkiwa na Roho Mtakatifu?
Hayo yamo katika Agano Jipya na Agano la Kale pia.
Huyo Periklitos (Ahmad au Muhammad) "atauhakikisha ulimwengu kwa
habari ya dhambi, na haki, na hukumu." Na ndio hivyo ilikuwa ni
Muhammad aliyedhihirisha ukweli wote wa Mwenyezi Mungu mmoja, asiyezaa wala
asiyezaliwa, na akawaokoa umma mzima wasimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu cho
chote, wala mtu ye yote. Ni yeye ndiye aliyewarejesha Wakristo kwenye
mafunzo ya Yesu na Musa kwamba Mwenyezi Mungu hana utatu, bali Mungu wao ni
Mungu mmoja kama alivyofunza Yesu (Tazama Marko 12.29), na kama
alivyoamrishwa Musa (Tazama Kutoka 20.3-4). Ni yeye ndiye
aliyemtoa Yesu katika matusi ya Mayahudi walipomshutumu kuwa ni mdanganyifu, na
matusi ya wanaojiita Wakristo kumzulia kuwa kafa kifo cha laana msalabani, na
kuwa yeye ni mungu wa bandia kama walivyo miungu ya washirikina makafiri.
Kweli yote imehakikishwa na huyo Periklitos, Muhammad, Roho wa
Kweli. Huyo ambaye "hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini
yote atakayoyasikia atayanena" hawezi kuwa Mungu,bali huyo ni Mtume wa
Mungu, Mtume ambaye ametuachia Kitabu kizima ambacho kila neno liliomo humo ni
neno alilolisikia kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe. Hicho ni Kitabu pekee
duniani, nacho ni Qur'ani. Na ni Mwenyezi Mungu katika Qur'ani ndiye
aliyesema:
(Qur'ani) As Saff 61.6
Injili
ya Mtakatifu Barnaba ambayo ilipigwa marfuku kwa amri ya Gelasius katika mwaka
496 B.K., karne nzima kabla ya kuja Nabii Muhammad s.a.w. inaeleza:
Injili ya Barnaba Sura 97
Imehaririwa
na kufasiriwa kutoka Muswadda uliopo katika Maktaba ya Vienna, Austria, na
Lonsdal na Laura, Oxford. Hii Injili ya Barnaba ndiyo inaaminiwa kuwa ni Injili
ya pekee iliyoandikwa na mwanafunzi wake mwenyewe Yesu. Zilizobaki
zimeandikwa na watu wengine baada yao hao wanafunzi kwisha kufa, lakini
yakatumiwa tu majina ya hao wanafunzi. Injili hii ilikuwa inakubaliwa
kuwa ni sahihi na Wakristo wa kwanza, na ikitumiwa katika kanisa la Alexandria
mpaka mwaka 325 B.K. Mwaka huo ndipo Baraza la Nikaia likaamua
kuzikubali hizi Injili nne za Mathayo, Marko, Luka na Yohana ziingizwe katika
Biblia kuwa ni maandiko matakatifu, na likapiga marfuku Injili nyenginezo, na
mojawapo ni hii ya Barnaba, kuwa ati si sahihi. Vitabu hivyo
vilivyokataliwa viliitwa Apokrifa, yaani vinavyofichwa, na hapo zamani
ye yote aliyeonakana navyo aliuwawa.
Injili iliyokubaliwa na Baraza kuwa ni sahihi, na iliyomo katika Biblia, Injili
ya Mathayo, nayo inatueleza kuwa Yesu alibashiri kutokea kwa Muhammad, ambaye
ni katika uzao wa Ismaili, anayefananishwa na jiwe liliokataliwa na
wajenzi. Pia Yesu alibashiri kuinuka kwa Umma wa Kiislamu
utakaopewa Ufalme wa Mungu, nayo yote hayo yakatimia:
Mathayo 21.42-44
Yesu
kwa maneno hayo tuliyoyanukulu anawaambia Waisraili:
"Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye
kuzaa matunda yake." Taifa la Israili halitazaa matunda
tena. Yesu alililaani. Twasoma katika sura hii hii ya 21 ya
Mathayo:
Mathayo 21.18-19
Wataalamu
wa Biblia wanakubaliana kuwa huo mtini ulionyauka, usioleta matunda yake, ni
taifa la Israili. Na hatuna haja kutafuta maoni ya mtaalamu ye yote kutufasiria
kuwa taifa lizaalo matunda lenye kubarikiwa ni taifa la Ismaili liliomzaa Mtume
Muhammad. Biblia yenyewe inatwambia kuwa Mwenyezi Mungu alimwambia
Ibrahim:
Mwanzo 17.20
Kwa
hivyo tunaweza kusema bila ya wasiwasi kuwa Yesu alikusudia kuwambia
Mayahudi: "Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu kwa kuwa nyinyi
mmeacha amri za Mwenyezi Mungu alizozileta Musa na nilizothibitisha mimi, na
ufalme huo watapewa taifa la Muhammad, mwana wa Ismaili, taifa liliobarikiwa na
Mwenyezi Mungu, lenye kufuata maamrisho yake kama alivyofundisha Ibrahim na
Musa na mimi na Manabii wote waliokuja kabla yangu mimi."
Kama alivyobashiriwa Nabii Ibrahim kuwa katika uzao wake kwa mwanawe Ismail
utatokea umma uliobarikiwa wenye kuleta matunda, kadhaalika alibashiriwa Nabii
Musa na Mwenyezi Mungu kwamba katika ndugu zao Wana wa Israili, yaani Wana wa
Ismaili, atatokea Nabii, naye ni Nabii Muhammad, ambaye Mwenyezi Mungu
anawataka viumbe wote wamuitikie na wamfuate. Na ye yote
"asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka
kwake." Kwa ukamilifu Mwenyezi Mungu alimwambia Nabii Musa haya:
Kumbukumbu la Torati 18.19-22
Zingatia
vyema: maneno hayo anaambiwa Nabii Musa a.s., naye ni Nabii wa Wana wa
Israili. Nabii anayebashiriwa hatotoka miongoni mwao Wana wa Israili,
bali miongoni mwa ndugu zao, yaani Wana wa Ismaili. Lakini Nabii
huyo hatokuwa kwa Wana wa Ismaili tu, bali hata wao Waisraili pia, kwani
Mwenyezi Mungu anawaambia: "Nitawaondokeshea", yaani
wao pia Wana wa Israili. Tena Mwenyezi Mungu anasema: "Mtu
asiyesikiliza mananeo yangu atakayosema yule (Nabii) kwa jina langu, nitalitaka
kwake." Ni dhaahiri kuwa yawapasa watu wote, mataifa yote,
wampokee huyo Nabii atakyetokea katika ukoo wa Ismaili.
Mungu anasema: "Nitatia maneno yangu kinywani mwake."
Kitabu gani ambacho kinadai, na madai yenyewe yakawa ya kweli, kuwa ni maneno
khasa ya Mwenyezi Mungu isipokuwa Qur'ani? Muhammad alikuwa ni mkalimani wa
Mwenyezi Mungu, akiyatamka tu yale yaliyokuwa yakifunuliwa
kwake; na waandishi waliokuwepo miongoni mwa wafuasi wake wakiandika na
wengine kuhifadhi kwa moyo maneno ya Mwenyezi Mungu wakati ule ule yeye Nabii
Muhammad alipokuwa akiyatamka. Mwenyezi Mungu anamuamrisha katika
Qur'ani:
(Qur'ani) Al Ahqaf 46.9
Mwenyezi
Mungu mwenyewe anawakabili kwa majadiliano wenye kutia shaka kuwa hii Qur'ani
ni maneno yake au la:
(Qur'ani) Al Baqarah 2.23-24
Kwa
muda wa miaka 1400 hapajatokea mwanaadamu wala jini aliyeweza kujibu hoja
hiyo. Qur'ani ndio muujiza wa kudumu milele. Huu si muujiza wa kusimuliwa
ya kwamba ulitokea, na watu wakazozana ulitokea kweli au haukutokea. Huu
ni muujiza uliobaki na utabaki ukionekana tangu siku ulipoteremka mpaka leo na
mpaka milele. Unaweza kuusoma leo, kesho, kesho kutwa na mtondogoo na daima
dawamu, na ukuathiri kwa ufasihi wake uliokuwa hauna mfano, utamu wa maneno
yake, ukakuongoza kwa ubora wa mafunzo yake, ukakusaidia kukabiliana na
ulimwengu wako, ukaondoa matatizo yako ya kidunia na ya kiroho, ukatengeneza
dunia yako na akhera yako.
Yamkinika kuwa mimi nikatuhumiwa kuwa imani yangu inanipelekea kuisifu hivi
Qur'ani, lakini hebu natuiachie kalamu ya Muingereza Mkristo, Edward Gibbon,
ambaye ni mtaalamu mkubwa wa historia, na bingwa wa uandishi, tuiache kalamu
yake isiyo na khofu wala mapendeleo ituhukumie. Gibbon ameandika:
Basi ni kitabu hichi ndicho kilichowafanya Waislamu wa zamani wa Vyuo vyao Vikuu
vya Cordova (katika Uspania), Cairo, Damascus na Baghdad wakawa ndio waanzishi
wa ilimu za Algebra, Alkimya (chemistry), Falaki (Astronomy)
na utibabu wa kisasa. Peke yake ni jambo la kustaajabisha kuwa mtu ambaye
mwenyewe alikuwa hajui kusoma wala kuandika, katika kaumu ya wajinga, amri ya
kwanza iliyofunuliwa kwake - si kusali,wala kutoa zaka, wala kutazama wagonjwa
na wazee, bali hata si kuamini Mungu mmoja, bali:
(Qur'ani) Al 'Alaq 96.1-5
Umma
uliokuwa mjinga, mabedui wa jangwani - hali yao haikukhitalifiana sana na
kabila yo yote ya Kiafrika yenye kutangatanga na mifugo yao, kama Wamasai,
ambao ndani yake waliokuwa wakijua kusoma na kuandika wakihisabika kwa vidole
vya mkono mmoja - Umma kama huo ukaamrishwa la mwanzo la kulifanya ni kusoma,
na Mwenyezi Mungu mwenye kutoa amri hiyo hakutafuta sifa kubwa kuliko
Aliyefundisha kwa kalamu, Aliyemfundisha mwanaadamu yale aliyokuwa
hayajui. Kama huu si muujiza upi mwenginewe? Hii ni Ishara kuwa
enzi mpya imekuja, enzi ya kusoma, enzi ya kalamu, enzi ya kutumia akili. Enzi
za kugeuza fimbo kuwa nyoka, kufufua walioonekana kama wamekufa, kugeuza maji
yakawa mvinyo na mazingaombwe kama hayo zimepita. Hayo labda yafanywe juu ya
jukwaa katika majumba ya tamasha kwa kuwastarehesha vijana. Lakini katika
mambo yaliyo na uzito kweli yahitaji masomo, kujifunza, na kufundisha kwa
kalamu. Huu wakati wa muujiza wa hichi Kitabu kilichoandikwa kwa kalamu na
kinachoweza kusomwa milele, na kila mwenye tatizo lake anaweza kulitatua kwa
kusoma na kuzingatia vilivyo yaliyoandikwa humu na mwenyewe Mwenyezi Mungu
aliyemuumba mwanaadamu kutokana na tone la damu, bali kutokana na mchanga
khasa. Zama za muujiza wa kutumia akili na masomo umefika.
Bila ya Qur'ani ilimu zote za Warumi, za Magiriki, za Waajemi, za India, za
China, za Misri, na za Iraq, zingelipotea kabisa, badala ya kuwa zimehifadhiwa,
na zikazidi kukuzwa na kuendelezwa na zikakabidhiwa ulimwengu huu wa leo.
Kila tunapoona neema ya uvumbuzi wo wote ambao tukafikiri kuwa ndio wa kisasa
na umetokana na Wazungu yafaa tushukuru kuwa lau kwamba ingelikuwa Qur'ani
haikuamsha ulimwengu, na wakazindukana Waislamu wakatuhifadhia yaliyopita na
wakayaongeza mengi sana yao wenyewe tunsingezipata hizi neema za leo, ikiwa ni
katika matibabu, ikiwa ni katika vipando, ikiwa katika makaazi, ikiwa katika
vyakula, ikiwa katika usafiri, na ikiwa katika fanni zo zote na ilimu zo zote
za sayansi. Kitabu hichi ndicho kilichowageuza waliokuwa wakiabudu
jua na mwezi na nyota na mawe na mito na miti na milima, kikawaambia kuwa
vyote hivyo na vyenginevyo vyote vimeumbwa ili vimtumikie mwanaadamu. Ni
Kitabu hichi kilichokomboa akili za watu zichungue mpaka katika sehemu ambazo
watu kabla yake hata hawajaziotea:
(Qur'ani) Ar Rahman 55.33
(Qur'ani) Al Baqarah 2.164
Vifungu
hivi viwili tu tulivyovinukulu hapa vyatosha kukupa mawazo vipi Qur'ani
ilizindua wanaadamu waliolala washughulikie ilimu, na uchunguzi, na utafiti na
uvumbuzi. Uropa iliolala katika Karne za Giza (Dark Ages)
ilizinduliwa na muamko wa Kiislamu katika kila ilimu. Katika vifungu hivi
tunaona mahimizo na ishara ya kuanzisha ilimu za anga (Space Sciences),
ilimu za matabaka ya ardhi na uvumbuzi wa maadini (Geology na Minerology),
Jiografia, ilimu ya unahodha (Navigation), ilimu ya hali za hewa (Meteriology),
na ilimu za zaraa (ukulima). Huu ni mfano mdogo tu; ni kama tone
katika bahari. Mwenye kuisoma Qur'ani kwa moyo safi na akili kunjufu
atagundua ndani yake uwongofu ambao haupati po pote kwengineko, atapata ilimu
ambazo hazipati po pote, na atapata ukunjufu wa moyo ambao hawezi kuupata
penginepo.
Ikiwa Mtume Muhammad alikuwa na sifa yo yote ambayo ilizagaa zaidi kuliko
nyengine basi ni hiyo sifa ya kubashiri jambo nalo likatokea kama
alivyosema. Hayo yajuulikana kikweli kwa kuwa maisha yake, kinyume na
waongozi wa dini zilizotangulia, yalikuwa katika zama ambazo zinajuulikana
vyema na wanachuoni wa taarikh (historia). Yeye si mtu wa hadithini,
lakini ni mtu wa hakika, anayejuulikana vilivyo, mtu aliyekuwa akikatibiana na
kupambana na wakuu wa serikali na dola zilizokuwapo zama zake.
Akikatibiana na Mfalme wa Uajemi, na Mfalme wa Rumi, na Wakuu wa Misri na
Uhabeshi, na Wakuu wengineo walioko Arabuni na nje ya Arabuni. Kwa kutimia
kauli zake, kama tulivyokwisha toa mifano kadhaa wa kadhaa, ndio akaitwa As
saadiq, Msema Kweli, Al Amin, Muaminifu.
Bishara aliyopewa Nabii Musa a.s. inasema: "Mimi nitawaondokeshea
nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe." Hakuja Nabii baada ya
Musa aliyefanana naye kama alivyofanana naye Nabii Muhammad. Musa na
Muhammad walikuwa wakhubiri wa dini kwa mambo ya kiroho, na vile vile wakawa ni
waongozi katika mambo ya dunia. Walikuwa wamekusanya dini na siasa,
Unabii na utawala, uwalii na uamiri jeshi. Walikuwa ni maraisi wa kaumu
zao, walikuwa mahakimu, walikuwa wapigania uhuru licha ya kuwa wanasiasa.
Nabii Musa alipambana na Firauni na kaumu yake, Muhammad alipambana na Abu
Jahli na kaumu yake. Musa ilimlazimu akimbie ahame Misri alikozaliwa ende
Palastina. Muhammad pia ilimlazimu aongoze watu wake kukimbia adhabu za
Makureshi Makka alikozaliwa ende Madina. Nabii Musa kapokea sharia ya Mungu
katika Taurati, na Nabii Muhammad kapokea sharia ya Mungu katika Qur'ani. Wote
wawili walioa wakawa na wake na wakazaa. Wote wawili walikufa kitandani
ulipotimia mwisho wa maisha yao.
Mwenyezi Mungu alimwambia Nabii Musa: "Lakini nabii atakayenena neno
kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena
katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa."
"Nabii yule atakufa." Nini maana ya haya? Kufa ni
faradhi kwa kila kilio hai. Maana yake atakufa siku si zake, yaani atakufa
ghafla naye kijana, au atauliwa. Nabii Muhammad alikufa na umri wake
miaka 63, kiasi ya umri wa utuuzima wakati ule na mpaka hivi sasa. Juu ya
misukosuko isiyokadirika, na vita alivyopambana navyo, na majaribio ya kumuua
aliyofanyiwa katika maisha yake, Mwenyezi Mungu alimsalimu mpaka akafika wakati
wake baada ya kutimiza na kukamilisha ujmbe wake aliyopewa, na akafa kitandani,
na huku kazungukwa na ahali zake. Yaliyosemwa katika Taurati pia yamesemwa
katika Qur'ani:
(Qur'ani) Al Haqqah 69.44-47
Ama
wanavyodai wengine kuwa bishara hii yamkhusu Yesu wamekosea sana. Yesu
hakufanana na Musa ila katika kuwa ni Nabii na kuwa ni Mwana wa Israili.
Kwa unabii wale wanaomdaia ungu Yesu wanamkatalia kuwa ni Nabii. Ikiwa
Yesu kafanana na Musa, basi si Mwana wa Mungu wala si Mungu. Kwa hivyo wanajipinga
wenyewe. Bishara inasema wazi kuwa huyo Nabii hatakuwa katika Wana wa Israili,
bali miongoni mwa ndugu zao, nao ni Wana wa Ismaili. Yesu ni Muisraili. Kwa
hoja hii pia Yesu siye aliyebashiriwa hapa. Nabii huyo aliyebashiriwa kama ni
wa kweli hauliwi, wala hafi kijana. Yesu, kama wanavyodai Mayahudi na
wakaamini Wakristo, aliuwawa msalabani, tena yungali kijana. Ikiwa
bishara hii wanataka kumuambatisha nayo yeye Yesu, basi itakuwa wanamtuhumu
kuwa Yesu ni nabii wa uwongo "aliyenena neno kwa kujikinai kwa jina la
Mungu, ambalo hakuagizwa kulinena." Mwenyezi Mungu apishe mbali. Zaidi
ya hayo Nabii Isa kinyume na Nabii Musa na Nabii Muhammad (rehema na amani ya
Mungu iwashukie wote) hakuja na sharia yo yote. Yeye alifuata ile ile sharia ya
Musa iliomo katika Taurati, na mwenyewe kasema yeye hakuja ila kutimiza tu.
Wala yeye hakuongoza watu katika mambo ya kilimwengu, bali alimwachia Kaisari
ulimwengu na yeye kashughulikia mambo ya akhera, ufalme wa mbinguni.
Miezi mitatu tu kabla ya kifo chake Mtume Muhammad s.a.w. aliyataja maneno ya
Mwenyezi Mungu aliyoteremshiwa:
(Qur'ani) Al Maida 5.3
Miaka
mia sita kabla ya haya Yesu naye alisema: "Chakula changu ni
kufanya mapenzi ya yeye aliyenituma na kutimiza kazi yake."
Wote wawili wamekutana kwenye kutenda apendayo Yeye aliyewatuma, na huo ndio
Utume, na huo ndio Unabii, na huo ndio Uislamu. Kutenda mapenzi ya
Mwenyezi Mungu ndio waajibu wa binaadamu, na katika hayo ndio hupatikana wema,
na katika hayo ndio kuhisabiwa haki katika maisha haya na maisha ya milele ya
baadaye. Huko ni kufuata mwenendo wa maumbile aliyowaumbia Mwenyezi Mungu
wanaadamu wote kama mwenyewe asemavyo:
(Qur'ani) Ar Rum 30.30