Yasemekana kuwa watu wote tangu Adam na Hawa wana dhambi kwa
kuwa wazee wao hao walimkosa Mungu kwa kwenda kula mti waliokatazwa. Kwa
hivyo wanamnyima Mungu sehemu ya haki yake. Hapana njia kuepukana na adhabu
isipokuwa kwa kumrejeshea Mungu kile alichokhasiriwa na wanaadamu. Hoja iliopo
ni kuwa ilivyokuwa wema wote uwezekanao kutendeka tokea hapo ni haki yake
Mungu, hapana faida ipatikanayo kwa kutengeneza makosa yakisha tendeka.
Kwa hivyo ni mtu kamili asiye na dhambi kabisa anayekubali kuadhibiwa kwa
madhambi ya watu wengine, ndiye awezae kumtuza Mungu kukasirika kwake.
Ilivyokuwa ni Mungu tu ndiye asiye na dhambi, basi ni Yeye ndiye yampasa
achukue umbo la mwanaadamu ajitolee, ajiachilie ateswe na auwawe kwa
makosa ya viumbe vyake.
Craveri anasema:
Hebu tuangalie hoja zinazotumiwa kutoka katika Biblia za kuleta imani ya
kuokoka kwa damu ya Yesu. Injili ya Marko inasema:
Marko 10.42-45
Kifungu hicho tulichokinukulu ni moja katika ushahidi unaotolewa katika thiolojia (ilimu ya Ungu) ya Kikristo kuthibitisha imani ya kuwa Yesu kaja duniani auwawe na damu yake iwe ni kafara au fidia kwa dhambi za wanaadamu. Hebu natukiangalie vyema kifungu hichi, chasema nini?
Katika
gazeti moja la Misri ilitoka picha ya kuchora ya kuwapiga vijembe wale
wanaotetea viti vya bunge. Picha ilionyesha mazishi. Watu wamechukua
jeneza ambalo limezungushwa bendera kubwa ilioandikwa: "Mtu
Anayekufa kwa Ajili Yenu". Utepe uliotatiza shada la mauwa
liliochukuliwa mbele ya jeneza uliandikwa: "Mpaka Makao yake ya Mwisho ya
Kupumzika, Kiti cha Bunge." Na mtu mmoja akisoma: "Mtilieni
Voti!" Katika wale wendao mazikoni mmoja lilimdondoka chozi, mwenzie
akamzindua:
"Jizuie, mwanamume wee! Hii na kampeni tu!"
Ikiwa basi Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi za watu, na ikiwa kweli
yeye ni Mungu, basi mambo yote hayo ni kama sarkasi tu, mchezo wa kuigiza, au
kiini macho. Kwani hakika Mungu haiwezi kuwa aliona uchungu kwa yale
mateso, na kufa kwake kulikuwa hakuna maana, kwani kumbe hakufa. Mungu
hufa? Yote hayo yaonyesha kuwa ni udanganyifu mkubwa.
Na ikiwa yote hayo yalikuwa yamekwisha kadiriwa tangu mwanzo na kupangwa na
kutimiza bishara za kinabii na kwa kupenda kwake Yesu, basi hao waliomtesa na
wakamwua yafaa wafikiriwe na watukuzwe kama ni watu wema waliowaletea kheri
wanaadamu wote, na wakamsaidia Yesu kutimiza lile alilolijia. Hao akina
Yuda, na Pilato, na lile baraza la wakuu wa Kiyahudi, wote hao ndio vipenzi vya
Mungu, waliotimiza mapenzi ya Mungu baraabara.
Kifungu kingine cha maneno ya Biblia kinachonukuliwa mara nyingi kutilia nguvu
imani ya kuokoka kwa damu ya Yesu ni hiki kutokana na Luka:
Luka 1.67-71
Bishara
hii ni ya Zakaria alipozaliwa mwanawe Yohana (Nabii Yahya). Lakini ni
wazi kuwa anasema ni Bwana Mungu ndiye aliyewaokoa watu wake kwa
"kuwasimamishia pembe ya wokovu", naye ni Masihi aliyekuwa
akitarajiwa na Mayahudi kuja kuwakomboa kutokana na adui zao wanaowachukia, nao
ni watawala wa Kirumi. Kuja huyo mwokozi, anasema Zakaria, ni kutimiza yale
maneno waliyoyasema manabii wa zamani. Ni kuyapotoa maana ya maneno
tukifasiri utabiri huu kuwa maana yake ni kuokolewa kwa damu ya Yesu.
Ushahidi mwingine unaodaiwa kuwa ni dalili ya uwokovu kwa damu ni huu:
Yohana 1.29
Hata
tukijaalia maneno haya ya Injili ya Yohana ni kweli (kwani hayathibitishwi na
Injili zote nyenginezo) basi si kama tunavyomtaja kiongozi ye yote wa kidunia
hivi leo kwa kusema: "Muangalieni huyo anayetubebea mizigo yetu
yote"? Au tunapomwonya mmoja wetu: "Baba, utajiua nafsi yako kutaka
kujitwika mambo ya ulimwengu mzima kwenye mabega yako hayo!" Kuchukua
dhambi si lazima iwe maana yake ni kusamehewa dhambi kwa kuuliwa Yesu; bali ni
kwa kuyafuata mafunzo yake na kwenda mwendo wake ndio watu watapata
uwokovu. Ni kwa kuyatenda mapenzi ya Mwenyezi Mungu aliyemtuma mtumishi
wake Yesu, kuwa ni Nabii na Mtume, kama mwenyewe mara nyingi alivyosema, ndio
watu wataokoka. Ni kwa kutenda mema na yaliyokuwa ya murwa kwa mujibu wa
mapendo na sharia za Mwenyezi Mungu ndio kila mtu ataweza kujiokoa nafsi yake.
Sifa, bila ya shaka, itamrejea yule mwenye kuonyesha njia, na kwa hakika hivyo
ndio amekuwa ni mwokozi wa watu. Mafunzo na maisha yake Yesu ndio muhimu yenye
maana, na ndio hayo amejia duniani. Ama mateso yaliyompata ni matukizi
yaliyomzukia katika ile kazi yake, wala yeye hakuyapenda; au asingekimbia na
kujificha na kumwomba Mungu amwondolee kikombe cha mateso na mauti.
Yatufalia basi kuyatupa kando yaliyo muhimu na yenye maana, na
tukan'gan'ganilia yaliyozuka tu?
Kifungu hichi kifwatacho kutokana na Injili ndicho kinachoonekana chenye
ushahidi mkubwa wa imani ya kuokoka kwa damu:
Yohana 3.16-17
Hapa
yafaa tutambue kuwa hii Injili ya Yohana ni khitilafu kabisa na zile nyengine
tatu. Hii iliandikwa mwishoni kabisa baada ya zile. Tangu awali
haikukusudiwa hii kuwa ni maelezo ya kweli kueleza maisha ya Yesu kama yalivyokuwa,
bali ilikusudiwa kuwa ni maoni ya huyo mwandikaji, naye amejaza humo mawazo
yake mwenyewe. Ni dhaahiri kuwa Injili ya Yohana ilikusudiwa kuthibitisha
imani ambazo alikuwa zilikwisha mvaa mwandikaji. Wakati ilipoandikwa Injili hii
Ukristo wa Paulo ulikuwa umekwisha pata nguvu na huyu mwandikaji alikuwa bila
ya shaka ni mfuasi wa Ukristo wa Paulo, sio ule wa Yesu uliokuwa ukifuatwa na
wanafunzi wake wa mwanzo. Katika Injili hii ungu wa Yesu unatiliwa mkazo, na
Yesu ndio anaitwa "Mwana wa pekee wa Mungu." Juu ya hivyo hii
imani ya kuokoka kwa damu hata katika Injili hii haikusemwa kwa uwazi. Sana
sana, itakuwa kama imegusiwa tu. Ni yule mtu ambaye akili yake tangu hapo
imekwisha pikwa ndiye atafasiri maneno haya:
"Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu,
bali ulimwengu uokolewe katika yeye," kuwa maana yake ni kwa kufa kwake
juu ya msalaba; au akafasiri "kila mtu amwaminiye" kuwa maana yake ni
kuamini kuwa kifo chake kitakuwa ni fidia kwa dhambi za watu.
Dr. Hugh Schonfield katika Those Incredible Christians anatueleza kwa
vizuri nini thamani ya Injili hii kama alivyoiandika Yohana katika
kusimulia maisha na mafunzo ya Yesu Kristo. Anasema: