Labda katika miujiza yote ya kumthibitishia Yesu ungu ni kule kuzaliwa kwake na bikra bila ya baba. Wengi wanaona hayo ndiyo yanayoonyesha kwa nguvu zaidi kuwa yeye ni Mungu au Mwana wa Mungu. Mtaalamu mkubwa wa Kikristo, Maurice Wiles, Professor of Divinity and Canon of Christ Church Oxford, na Mwenyekiti wa Tume ya Imani ya Kanisa la Kiingereza, ameeleza vipi ilivyokuwa ni muhimu kabisa kuamini kuzaliwa na bikra kwa mwenye kutaka kuamini kwamba Yesu ni Mungu. Professor Wiles akiandika katika kitabu The Myth of God Incarnate (Uwongo wa Mungu kuwa Mtu) amesema:
"Mwanzoni mwa karne hii (ya ishirini) zilipokuwa shaka shaka zinatamkwa kuwa ati ni kweli hakika Yesu alichukuliwa mimba na bikra, maneno hayo ya kuonyesha shaka yalionekana mara nyingi kuwa ni mashambulio khasa juu ya imani ya kuwa Mungu kawa mtu. Ilionekana kwamba imani ya kuzaliwa na bikra na kwamba Mungu amekuwa mtu ni kama pacha wasiobandukana, ama zitasimama pamoja au zianguke pamoja."
Biblia yasemaje juu ya jambo hili? Kwa hakika si kitu cha kawaida mtu
kuzaliwa na mwanamke bikra asiyeingiliwa. Ni kweli huo ni muujiza. Lakini ndio
ndivyo kuamini kuwa chenye kuzaliwa kwa muujiza ni Mungu? Au hata ndio
ndivyo kuona tukio kama hilo ni dalili mojawapo ya kuzidisha ushahidi ya kuwa
huyo mtoto ni Mungu au Mwana wa Mungu, kwa maana wanavyotaka wakuu wa makanisa
wafwasi wao waamini?
Biblia inayotwambia kuwa Yesu kazaliwa bila ya mama yake kuingiliwa na
mwanaadamu (Injili ya Mathayo 1.18) vile vile inatuambia ya kuwa Adamu
hakuwa na baba wala mama. (Mwanzo 1.26- 27). Kama wa Yesu ni muujiza wa
Adam ni muujiza mardufu. Hali kadhaalika Paulo amewaandikia Waebrania:
Waebrania 7.1-3
Tunaona
basi Biblia inatuhakikishia kuwa Yesu hakuwa pekee mwenye kuzaliwa bila ya
baba. Wapo waliomtangulia katika muujiza huu. Kama huo ndio ungu, basi
wangelikuwa Adam na Melkizedeki wa mbele, ambaye anasimuliwa na Biblia kuwa
alikuwa
Hoja nyingi zimetolewa kukanya fikra ya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aligeuka
binaadamu akaishi duniani kwa sura ya Yesu wa Nazareti. Hoja hizo ziko za
misahafuni mpaka za kisayansi. Katika Qur'ani ameshabihishwa Yesu na Adam. Hali
kadhaalika muujiza ulitokea kabla kidogo tu ya kuzaliwa Yesu, alipochukua mimba
Elizabeti, mke wa Zakaria na ilhali huyo mama ni tasa tangu ujana wake na hapo
kesha zeeka na kapindukia miaka ya kuzaa. Mumewe, naye, Zakaria alikuwa ni
mkongwe. Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'ani, Sura ya Al Imran:
(Qur'ani) Al Imran 3.40
Ilipofika
zamu ya Maryam kuchukua mimba Qur'ani inasema:
(Qur'ani) Al Imran 3.47
Hizi ni
hoja za misahafu, ni hoja za watu wenye imani. Wapo wengineo ambao wamepuuzilia
mbali hadithi yote hiyo ya kuwa Maryam kachukua mimba bila ya kuingiliwa na
mtu. Hao ni kama Mayahudi ambao wanamtukana Yesu na mama yake kwa kusema kuwa
hiyo ni mimba ya haramu. Miongoni ya wataalamu wa Kizungu wenye asli ya
Ukristo wapo wanaoamini hayo. Wanasema kuwa imani ya kuzaliwa na mama bikra
ilikuwako tangu zamani katika dini za kipagani (kishirikina) kabla ya kuja
Yesu. Bikra Rea Silvia alimzaa Romulus wa Roma. Horus wa Misri alizaliwa na
Isis, malkia bikra wa mbinguni. Hoja inayotolewa kama ilivyokuwa hizi na
nyenginezo ni hadithi za kubuni tu zilioenea pande za Bahari ya Kati, basi ndio
hivyo hivyo hadithi ya kuwa Maryam alikuwa bikra alipochukua mimba na kumzaa
Yesu ni hadithi ya kubuni kuiga zile zilizotangulia.
Mtaalamu wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri anawashutumu wakuu wa Kanisa
kwa kutafuta kila kipengee katika Biblia kutoa ushahidi kuwa kuzaliwa kwa Yesu
na bikra kuliaguliwa mbele. Kipande kinachonukuliwa mno ni kile kiliomo katika
Isaya ambacho kinasema:
Isaya 7.14
Mtaalamu
huyu anasema maneno haya hayakukhusu kuzaliwa kwa Yesu hata chembe. Kwanza neno
la asli halikutaja "bikira" lakini ni "mwanamke
kijana". Tafsiri nyingine
Mtaalamu mwengine mwenye kupima mambo kiakili aitwaye G. Vermes amesema katika
kitabu chake Jesus the Jew (Yesu Myahudi) akidai kuwa hili neno "bikira"
hata lilivyotumiwa kwa Mariamu yawezekana sana kuwa maana yake ni kuwa mdogo
mno kwa uzazi, kama walivyokuwa Sara, Hanna na Elizabeti kuwa ni wakongwe mno,
au tasa.
Mwishoe kuna maoni ya mwana-sayansi na daktari juu ya hili suala la kushika
mimba mwanamke hali naye ni bikra. Dr. T.H. Van de Velde M.D. akiandika katika
kitabu chake cha kitaalamu, Ideal Marriage (Ndoa Bora) anasema:
Hapana shaka pana utaalamu mkubwa katika mawazo na fikra hizi, za kidaktari, za
kisayansi au za kiakili; lakini ni Qur'ani ndiyo inauweleza ukweli kwa maneno
mepesi kabisa hata watoto wachanga wakaweza kuelewa na ikawa ya kuwatukuza Yesu
na mama yake:
(Qur'ani) Al Imran 3.59-60