Katika Agano
la Kale kitabu cha kwanza, kinachoitwa Mwanzo, imo hadithi ya kuumbwa mtu na
kuanguka kwake. Hivyo ndivyo inavyosimuliwa alivyoanguka Adam kutokana na
kukosa neema:
Mwanzo 2.15-17
Juu ya
hivyo lakini Adam kwa kushawishiwa na mkewe, Hawa, aliasi amri ya Mungu na
akala matunda ya mti wa ujuzi aliyokatazwa. Mungu akawalaani wote wawili:
Mwanzo 3.16-19
Kwa
ajili ya dhambi yao hiyo, Kanisa linasema, Adamu na Hawa wakakosa neema ya
kutakaswa, haki ya kuwapo Mbinguni na vile vipawa vyao mahsusi; ndio
ikawa waweza kufa, kuteseka, na kuwa na matamanio makubwa kutenda maovu na
wakafukuzwa kutoka bustani ya Paradisio (Firdausi). Kwa sababu ya dhambi
ya Adamu wanaadamu wote wakizaliwa wanakosa neema ya utakaso na wanarithi
adhabu yake. Hii ndiyo inayoitwa dhambi ya asili.
Thiologia, yaani ilimu ya Ungu, ya Mtakatifu Paulo iliikuza hiyo imani ya
Dhambi ya Asili kuthibitisha imani nyengine, yaani imani ya kuokoka kwa kifo
cha Yesu msalabani. Katika barua yake aliyowapelekea Warumi Paulo aliandika
hivi:
Warumi 5.12-15
Pia
vile vile Paulo aliwaandikia Wakorintho:
1 Wakorintho 15.22
Paulo
anakusudia kusema kuwa wanaadamu wote, wameingia makosani kwa vile Adam
alivyovunja amri ya Mwenyezi Mungu, ndio maana ya kufa kwao; mpaka kufa na
kufufuka kwa Yesu Kristo ndiko kumeleta uhai kwa wenye kumuamini kuwa yeye ni
Mwana wa Mungu aliyekuja duniani kwa ajili ya kuwaokoa walimwengu kwa kuteswa
na kutundikwa msalabani na kufa na kuingia Jahannam na kisha kufufuka na kupaa
mbinguni. Haya ni mafunzo ambayo Paulo amejaribu kufunza katika barua
zake. Lakini imani aliyofunza Paulo ya Dhambi ya Asili ya kurithiwa
inapingwa na vifungu vingine kutokana na Biblia. Katika Kumbukumbu la
Torati, kwa mfano (na hicho ni katika vitabu vitano vinavyohisabiwa kuwa ndiyo
Torati inayoaminiwa na Mayahudi na Wakristo) Musa anasema:
Kumbukumbu 24.16
Hali
kadhaalika tunasoma neno la Mungu katika kitabu cha Yeremia:
Yeremia 31.29-30
Tena
Neno la Mungu linaendelea kusema katika kitabu cha Ezekieli kwa uwazi zaidi:
Ezekieli 18.19-20
Hayo
tuliyoyanukulu kutokana na vitabu vya Yeremia na Ezekieli ni maneno ya Bwana
Mungu, na yale yaliyotoka katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati ni maneno ya
Musa, ambaye alileta sharia itokayo kwa Bwana Mungu na ambayo Yesu alisema kuwa
yeye hakuja kuitengua hata nukta moja bali amekuja kuitimiza tu. Ni wazi kabisa
kuwa nadhariya ya Paulo ya dhambi ya asili ya kurithiwa inagongana na neno la
Mungu kama lilivyo katika Biblia. Na haya yametajwa na Mwenyezi Mungu katika
Qur'ani:
(Qur'ani) An Najm 53.36-40
Katika
Injili pia upo ushahidi ya kuwa Yesu mwenyewe anapinga hiyo nadhariya ya imani
ya Dhambi ya Asili, yaani wanaadamu wamerithi dhambi aliyotenda Adam:
Yohana 9.1-3
Neno
"Rabi" kama lilivyo hapo juu kuitwa Yesu maana yake kwa lugha
ya Kiyahudi ni Maalim au Shekhe, sio kama wanavyotumia Waislamu kuwa ni Mola
Mlezi. Hata katika Kiarabu pengine hutumiwa kwa maana ya "bwana",
kama kusema: Rabbi lbait, yaani Bwana wa nyumba.
Kinyume na mafunzo ya Kanisa linalojiita kwa jina lake, ya kwamba watoto wote
waliozaliwa wamezaliwa katika dhambi, mwenyewe Yesu Kristo anathibitisha kuwa
watoto hawana dhambi. Tunaona hayo zaidi katika maneno haya yaliyotajwa katika
Injili ya Mathayo:
Mathayo 18.2-3
Maana
ya maneno hayo ya Yesu ni kuwa vitoto havina dhambi ya kurithi wala yo yote.
Kwa hivyo nini linalolazimisha kuwa mtoto hataokoka ila abatizwe? Au kuwa kila
mtu anahesabiwa kuwa ana dhambi mpaka aamini kuwa Mwenyezi Mungu kamgeuza
mwanawe wa pekee auliwe kama dhabihu kondoo imwagike damu yake, ndio Mwenyezi
Mungu awe radhi na amsamehe huyo mwenye dhambi? Huyu ni Mungu mwenye
rehema na mapenzi kwa viumbe vyake, au ni Mungu aliye katili kwa waja wake na
hata kwa mwanawe? Kwanza awasingizie wanaadamu wote kuwa wana dhambi kwa
jambo wasilolitenda, kisha kuwasamehe kwake ni kwa kumwuua mwanawe mwenyewe!
Makosa mawili hayafanyi moja lisibu.
Basi tunaona kuwa nadhariya ya imani ya kuwa dhambi hurithiwa iliyoanzishwa na
Mt Paulo kama ilivyo katika barua yake ya mwanzo kwa Wakorintho tulionukulu
hapo juu, inapingwa na ushahidi wenye nguvu zaidi kutokana na Biblia, yaani kwa
maneno ya Musa yaliyomo katika Kumbukumbu la Torati, na maneno ya Bwana Mungu
yaliyomo katika Yeremia na Ezekieli, na maneno ya Yesu kama yaliyomo katika
Injili ya Mathayo na Injili ya Yohana. Lakini wazee wa Kanisa wamekhiari
kuukataa ushahidi wazi wa kukata wa Nabii Musa, wa Bwana Mungu, na wa Yesu,
uliomo katika Torati na Manabii na Injili, na kufuata badala yake ubishi wa
barua za Mt Paulo. Lakini huyo Mtakatifu Paulo ni nani?