Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani  (Nani Yeye?)

 

113. SURAT AL-FALAQ

(Imeteremka Makka)

 

Sura hii inamtaka Nabii s.a.w. amwendee Mola wake Mlezi atake ulinzi kwake kujilinda na shari ya kila mwenye shari, ya viumbe vyake, na shari za usiku linapo ingia giza, yanayo yasibu nafsi katika hali ya upweke, na madhara ambayo mtu hawezi kujikinga nayo, na shari za mafisadi wanao pita kuharibu makhusiano na mawasiliano yalio baina ya watu, na shari za hasidi anaye tamani kuondoa neema alizo wapa Mwenyezi Mungu waja wake.


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko, Maelezo

2. Na shari ya alivyo viumba, Maelezo

3. Na shari ya giza la usiku liingiapo, Maelezo

4. Na shari ya wanao pulizia mafundoni, Maelezo

5. Na shari ya hasidi anapo husudu.  Maelezo  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani