Qur'ani Tukufu

Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani (Nani Yeye?)

 

105. SURAT AL-FIIL

(Imeteremka Makka)

 

Mwenyezi Mungu anampa khabari Mtume wake s.a.w. kisa cha Watu wa Tembo (Ndovu) walio kusudia kuivunja Nyumba ya Mwenyezi Mungu ya Al-Kaa'ba, na anakionyesha kisa hichi kuwa ni dalili ya uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kujilipizia kwake juu ya hao wanao vunja vitu vyake vitakatifu. Mwenyezi Mungu hakika aliwasalitishia majeshi yalio wang'oa mizizi yao, na wasibakie kitu ila kama nazi iliyo liwa na mwezi.


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? Maelezo

2. Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Maelezo

3. Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Maelezo

4. Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Maelezo

5. Akawafanya kama majani yaliyo liwa!  Maelezo  


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejea uliko toka

Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com

Copyright 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani